Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama)
akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (hawapo
pichani) wakati wa mkutano uliotishwa na Tume hiyo jana jumapili tarehe
14. Oktoba, 2012 katika Ukumbi wa Mikutano wa Baraza hilo mjini
Zanzibar, uliolenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu mchakato wa
Mabadiliko ya Katiba. Kutoka kulia ni Wajumbe wa Tume hiyo, Profesa
Paramagamba Kabudi, Suleiman Ali, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Ali Abdalla Ali, Mjumbe wa Tume Joseph Butiku, Katibu wa Tume
Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.
Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakifuatilia kwa makini mkutano wa
kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, uliofanyika jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012 katika ukumbi
wa mikutano wa Baraza hilo mjini Zanzibar , ambapo wajumbe hao walipata
fursa ya kutoa maoni yao kwa Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya
Katiba.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja Zanzibar
ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Shamsi
Vuai Nahodha , akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano
ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi jana jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, uliolenga kukusanya
maoni ya Wajumbe wa Baraza hilo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Asha Bakari Makame akitoa maoni
yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana
jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya
Wajumbe hao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Utalii na Michezo, Mhe. Said Ali Mbarouk, akitoa maoni yake kuhusu
Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe 14.
Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu
mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
Mhe.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho
(aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
(hawapo pichani) wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana
jumapili tarehe 14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya
wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Kulia ni Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba na Mjumbe wa Tume Joseph Butiku.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongozwa
na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho
(kushoto), kuwaaga wajumbe wa Baraza hilo mara baada ya kumalizika kwa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo mjini
Zanzibar jana jumapili tarehe 14. Otoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya
maoni ya Wajumbe hao kuhusu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Mwakilishi
wa Jimbo la Mji Mkongwe, Mhe. Ismail Jussa Ladhu akitoa maoni yake
kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano uliotishwa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba katika ukumbi wa mikutano wa Baraza hilo jana jumapili tarehe
14. Oktoba, 2012, ambao ulilenga kukusanya maoni ya Wajumbe hao kuhusu
mchakato wa Mabadiliko ya Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment