Bondia
Thomas Mashali kulia akiwa amesimama na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoani ACP Charles Kinyela, Rais wa Shirikisho alNgunu la ECAPBA
Onesmo Ngowi na Mbunge wa Kinondini Idda Azan.
Shirikisho la Ngumi
za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) limempongeza bondia
Mtanzania Thomas Mashali kwa kushinda ubingwa wa ECAPBA katika uzito wa
kati (middleweight) uliokuwa wazi jana tarehe 14 Octoba.
Mpambano
huo uliomkutanisha Thomas Mashali na Sebyala Med toka Uganda na
ulifanyika katika ukumbi wa Friends Corner, Manzese katika wilaya ya
Kinondoni na kuhudhuriwa na maelfu ya Watanzania pamoja na wageni toka
nchi jirani.
ECAPBA
inatambua na kuenzi kipaji alichoonyesha bondia Thomas Mashali na
kumtakia kila la kheri katika maisha yake kama bingwa halali wa ECAPBA.
Mpambano
huo uliandaliwa na promota Seleman Simunyu na kusimamiwa kwa
ushirikiano wa pamoja kati ya TPBC na TPBO. Kamishna wa mpambano alikuwa
ni Boniface Wambura ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Viwango na
Ubingwa wa TPBC, refarii alikuwa Nemes Kavishe ambaye ndiye Katibu Mkuu
wa TPBC, Jaji namba 1 alikuwa Mark Hatia wa TPBC, Jaji namna 2 alikuwa
aid Chaku ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi wa TPBO na jaji namba 3 alikuwa
Sake Mtulya wa TPBO.
Bingwa Thomas Mashali anatakiwa akae na ubigwa huo kwa kipindi cha miezi sita na kuutetea kabla kipindi hicho hakijamalizika.
Aidha
ECAPBA linampongeza Rais wa TPBO Yasin Abdallah (Ustaadh) kwa kazi
nzuri aliyofanya kusimamia utaratibu mzima wa mpambano huo!
Shirikisho
la Nguni za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) lina
wanachama toka nchi zifuatazo: anzania, Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini,
Ethiopia, Malawi, Rwanda, Burundi, DRC Congo na Zambia.
No comments:
Post a Comment