Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati (KAGAME),timu ya Yanga imeendelea na mazoezi leo
asubuhi katika Uwanja wa shule ya sekeondari Loyola tayari kwa ajli ya
kuikabili timu ya Mgambo JKT siku ya jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi
cha wachezaji 20 na Benchi la Ufundi 7 kilirejea jana jioni kutokea
jijini Arusha ambapo katika mchezo wake dhidi ya timu ya JKT Oljoro
ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao lililofungwa
na mlinzi wa kati Mbuyu Twite dakika ya 53.
Wachezaji
wote wamefanya mazoezi asubuhi ya leo, kitu ambacho kocha Ernie
amefurahia kutokua na majeruhi hivyo anamini kikosi chake kiko tayari
kuivaa timu ya Mgambo JKTkatika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Kwa
matokeo hayo, Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara kwa pointi 20, ikiwa nyuma ya watani wa jadi
Simba wenye pointi 22 huku waoka mikate timu ya Azam FC ikiwa katika
nafasi ya nne, baada ya timu ya Coastal kushinda jana na kufikisha
pointi 19.
Kocha
mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahishwa na
mabadiliko ya kiuchezaji ya kikosi chake,kwani wachezaji wake kwa sasa
wanaonyesha kumuelewa anavyotaka wacheze,hivyo anaamini mabadiliko mengi
yataonekanakadri siku zinavyokwenda.
Brandts
ameongeza kwamba anapenda wachezaji wake wacheze pasi za haraka haraka
huku wakipanga mipango ya mashambulizi, na kwa sasa anaona wachezaji
wanaanza kumuelewa hali inayopelekea timu kuibuka na ushindi wa 4
mfululizo.
Katika
michezo itakayochezwa siku ya jumatano, endapo Yanga itashinda na Simba
ikatoka sare basi Yanga itakamata usukani wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara
Young
Africans imebakisha michezo michezo 3 kabla ya kumalizika kwa duru la
mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
No comments:
Post a Comment