Baada ya kufungwa na Serena katika fainali ya WTA jumapili hii kwa seti 6-4,6-3 Maria Sharapova amekiri kuwa Serena ndiye anastahili kuwa mchezaji No.1 wa kike kwasasa katika Tenesi.
Pamoja na kushinda mataji makubwa manne  kwa mwaka huu, mchezaji bora kabisa wa tenisi kwasasa Serena Williams ameshindwa kuwa World No. 1 baada ya kutoshiriki mataji ya lazima ya WTA mjini Beijing na Indian Wells.
Iwapo Serena ageshiriki mataji hayo mawili angeweza kuwa World No1 kwakuwa amekuwa akimfunga Victoria Azarenka (world No1) katika michezo mitano mfululizo waliyo kutana mwaka huu, vivyo hivyo kwa Maria Sharapova (world No.2) aliyemfunga mara tatu mfululizo.