Jared
Loughner amehukumiwa kwa mauwaji ya watu sita ambaye pia alimjeruhi
vibaya Mbunge katika bunge la Marekani Bibi Gabrielle Giffords katika
tukio alilolifanya mwezi Januari mwaka jana. amehukumiwa vifungo saba
vya maisha pamoja na miaka 140 gerezani.
Mtuhumiwa
huyo Jared Loughner mwenye umri wa miaka 24 amehukumiwa vifungo saba
vya maisha pamoja na miaka 140 gerezani, hukumu hiyo ni baada ya kufikia
makubaliano na waendesha mashitaka mwezi Agosti ambayo yalimnusuru na
adhabu ya kifo.
Amekiri
kwenda katika eneo la maduka la Tucson, Arizona ambako watu walikuwa
katika tukio moja akiwa na mpango wa kumuuwa Giffords. Shambulizi hilo
lilimuacha katika hali mbaya Bibi Giffords kwa kumjeruhi kichwani,
kumsababishia ashindwe kuongea, kupooza mkono wa kulia pamoja na
kupoteza uwezo wa kuona vizuri. Giffords alikuwepo mahakamani wakati
hukumu hiyo inatolewa.
No comments:
Post a Comment