Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu  maswali ya papo kwa hapo  Bungeni mjinni Dodoma leo. 
Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakitoka kwenye ukumbi wa Bunge Mjini  Dodoma, Novemba 1, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Amani  na utulivu uliopo hapa nchini Tanzania utazidi kudumishwa daima  ikibidi kwa njia yeyote  na watanzania wawe na amni na kufanya kazi zao bila kuwa na wasiwasi  wowote.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliwahakikishia watanzania leo wakati akijibu maswali ya wabunge  mjini Dodoma katika kikao cha tatu la Bunge la Kumi kinachoendelea mjini Dodoma.
 Pinda amesema kuwa kama kuna mtu anadhani kuwa kwa kuleta chokochoko yake ataondoa amani na utulivu  uliopo hapa nchini Tanzania, basi mtu huyu anajisumbua na hayuko sahihi hata kidogo.
 Amesema kuwa ni kweli  kuna baadhi ya watu wengine wanajipatia kipato  kwa kutaka kiuanzisha fujo za kidini, watu wa aina hiyo tunawajua kwa sura na majina yao. Waziri ameahidi kuwachuklia hatua kali za kisheria na kuwafikisha mahakamani.