CAF imetangaza
orodha fupi ya majina ya wachezaji ambao wamo katika nafasi nzuri zaidi
ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora zaidi barani Afrika. Mshindi wa mwaka
jana, Yaya Toure, anaongoza katika orodha hiyo yenye majina ya wachezaji
10, waliochaguliwa kutoka orodha ndefu ya wachezaji 34.
Mchezaji
huyo kutoka Ivory Coast, ambaye ni kiungo cha kati wa timu ya Manchester
City, ni kati ya wachezaji wanne wanaozichezea timu za Uingereza ambao
huenda wakapata tuzo hiyo ya mwaka 2012. Kiungo cha kati wa Chelsea,
John Obi Mikel, mshambulizi wa Arsenal, Gervinho, Demba Ba wa timu ya
Newcastle, ni kati ya wachezaji wengine wa ligi kuu ya Premier ambao
wanawania tuzo hiyo.
Katika
orodha hiyo, kuna wachezaji wengine ambao waliwahi kucheza Uingereza
mwaka 2012. Wachezaji hao ni aliyekuwa kiungo cha kati wa Arsenal,
Alexandre Song, na ambaye sasa huichezea Barcelona ya Uhispania, na
mshambulizi wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba, ambaye anaichezea klabu
ya China, Shanghai Shenhua.
Chris
Katongo ni mchezaji wa pekee kutoka timu ya Zambia iliyoibuka mshindi
katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Mchezaji wa Morocco,
Younes Belhanda, yumo katika orodha hiyo, kwa juhudi zake mapema mwaka
huu, katika timu ya Ufaransa ya daraja ya kwanza, Montpellier.
Wanaowania
tuzo hiyo, watapunguzwa hadi kufikia watatu, katika wiki ya mwisho ya
mwezi Novemba. CAF vilevile ilitangaza orodha fupi ya wachezaji watano,
ambao wana nafasi ya kupata tuzo la mchezaji bora barani Afrika, kwa
wachezaji ambao hucheza kandanda yao barani Afrika.
Katika
ordha hiyo ni pamoja na Mohamed Aboutrika, kiungo cha kati kutoka Misri,
na aliyecheza katika mechi ya Al Ahly ya klabu bingwa dhidi ya
Esperance ya Tunisia, mchezo uliokwishwa kwa sare ya 1-1 siku ya
Jumapili.
Tuzo
hizo, ambazo zitakuwa pia ni kumpa zawadi kocha bora zaidi wa mwaka, na
klabu bora zaidi mwaka 2012, zitatolewa kwa washindi tarehe 20 mwezi
Desemba, katika ukumbi wa Banquet, katika ikulu ya rais, katika mji mkuu
wa Ghana, Accra.
-BBC
-BBC
No comments:
Post a Comment