Maiti ya Kijana Rashid Juma aliyepigwa risasi
na askari polisi ikiwa imelazwa katika chumba cha kuifadhia katika hospitali ya
Wilaya ya Bukombe.
BUKOMBE
Mtu mmoja anayeitwa
Rashid Juma (23) ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi katika kitongoji
cha Kilimahewa kilichoko mjini Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoani Geita leo(Nov 24) Asubuhi.
Marehemu Juma amedaiwa
kupigwa risasi na askari polisi wakati walipokuwa wanakamata mtu, anayesadikiwa
kuwa ni jambazi, aliyekuwa amejificha kwenye nyumba moja katika kitongoji
hicho.
Mwandishi wetu
ameripoti kuwa, baada ya askari kumtia mbaroni mtuhumiwa huyo, wananchi wenye
hasira walilivamia gari la polisi kwa nia ya kumuua, hali iliyosababisha askari
waanze kupiga risasi za juu ili kuwatawanya.
Imeelezwa kuwa katika
tafrani hiyo, marehemu aliokotwa na wananchi akiwa amejeruhiwa kiunoni kwa kitu
kinachohisiwa kuwa ni risasi ya moto, kabla ya kubebwa na wananchi hao kwa
maandamano hadi kituo cha polisi.
Mganga Mkuu wa Wilaya
hiyo Dk. Archard Rwezahura ameleza, marehemu Juma amefariki kabla yakufikishwa
hospitalini hapo na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Geita Lenard Paul amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba hatua
za kisheria zinafuatiliwa.
MATUKIO KATIKA PICHA
Askari polisi akijitahidi kuwatawanya
wananchi waliokuwa na hasira
Moshi
wa bomu la machozi ambalo lililirushwa na askari polisi wa kituo hicho kwa
ajili ya kuwatawanya wananchi ambao walikuwa na lengo la kuvamia kituo.
Msafara wa Mbunge, wa Bukombe, Profesa Kulikoyela
Kahigi Pamoja na Diwani na baadhi ya askari na wananchi wakiwa wanaongozana
kwenda katika hospitali ya Wilaya ya Bukombe kwa ajili ya kuangalia mwili wa
marehemu Rashid Juma aliyepigwa risasi na polisi na kufa hapo
Mbunge wa Bukombe Profesa, Kulikoyela Kahigi
Chadema (Kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya
Bukombe Dk. Archard Rwezahura, (aliyevaa shati la kitenge) jinsi alivyopokea
maiti ya kijana huyo ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufikishwa hospitali
hapo akiwa amefariki.
SOURCE SHOMARI BINDA BLOG
No comments:
Post a Comment