Rais
Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha mjumbe wa tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jaji Mstaafu John Mkwawa pamoja na Katibu wa Tume ya
Kurekebisha sheria Bi.winfrida Beatrice Korosso katika hafla
iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. Pichani juu
ni mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu John Mkwawa(8724)
na chini ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Bi.Winfrida Beatrice
Korosso(8734) Wakila kiapo mbele ya Rais leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Novemba 26, 2012 amewaapisha Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya
Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Katika
sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Jaji Mkuu,
Mheshimiwa Mohamed Chande Othman, Rais Kikwete amewaapisha Jaji Bethuel M.K. Mmilla na Jaji Ibrahim Juma kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Rais
Kikwete aliwateua Majaji hao tokea Oktoba 25, mwaka huu wa 2012, na
kabla ya uteuzi wake, Jaji Bethuel M.K. Mmilla alikuwa Jaji wa Mahakama
Kuu kwa miaka kumi tangu Juni 02, 2002. Vile vile, Jaji Mmilla amekuwa
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kwenye vituo vya Sumbawanga, Arusha na
Mbeya.
Naye Jaji
Ibrahim Juma kabla ya uteuzi wake alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya
Kurekebisha Sheria tangu mwaka 2007 na pia Jaji wa Mahakama Kuu tangu
Juni, 2009. Pia amewahi kuwa Mkuu wa Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, kati ya mwaka 2003 na mwaka 2006.
Katika hafla
tofauti iliyofanyika hapo hapo Ikulu leo, Rais Kikwete amemwapisha Jaji
Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa John Mkwawa kuwa Mjumbe
wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na amemwapisha Bi. Winfrida Beatrice
Korosso kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.
……..Mwisho………..
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
26 Novemba, 2012
No comments:
Post a Comment