MBUNGE
wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amesema yupo tayari kuipa
Serikali wachunguzi wa kimataifa iwatumie kuchunguza Watanzania
walioficha fedha haramu kwenye Benki za Uswisi.
Kauli
hiyo ya Zitto imekuja takriban wiki moja tangu alipoieleza Serikali
kwamba kama imeshindwa kuwachunguza walioficha fedha Uswisi, iwaachie
wenye uwezo wa kufanya suala hilo yenyewe isubiri majibu kwa manufaa ya
nchi.
Zitto
ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema kauli ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika kuwataka Watanzania
kupeleka majina ya vigogo walioficha mabilioni kwenye benki hizo ili
wachunguzwe, inaingilia uhuru wa Bunge na kwamba alitakiwa kuzungumza
jambo hilo bungeni.
Pia,
alisema lingekuwa jambo la busara kama Spika wa Bunge, angeweka wazi
ripoti ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge
kujihusisha na vitendo vya rushwa, ili umma uweze kufahamu kwa undani
juu ya uchunguzi huo.
Akizungumza
na Mwananchi Dar es Salaam jana, Zitto alisema kutaja majina ya
Watanzania hao siyo suluhisho, kinachotakiwa ni nchi kuwa na utaratibu
mzuri wa kubaini fedha zinazofichwa nje na kusisitiza kuwa siyo lazima
iwe Uswisi. Alisema Desemba 10, mwaka huu anatarajia kwenda Uswisi
kukutana na watafiti wake, huku mmoja akiwa anatokea Uingereza na
kwamba, atawapatia taarifa ya mahali taifa lilipofikia kuhusiana na
fedha hizo.
“Ni muhimu kuacha uchunguzi ukafanyika ili kuwabaini waliohusika kuliko kutaja majina ya watu. Ninaweza kutaja majina watu wakasema natafuta umaarufu,” alisema Zitto na kuongeza:
“Ni muhimu kuacha uchunguzi ukafanyika ili kuwabaini waliohusika kuliko kutaja majina ya watu. Ninaweza kutaja majina watu wakasema natafuta umaarufu,” alisema Zitto na kuongeza:
“Nikionana
na watafiti hawa nitawaomba kama watakuwa tayari kutoa ushirikiano na
timu ya uchunguzi inayofuatilia suala hilo, moja ya jambo ambalo
nitawaomba ni kutoa ushirikiano wao kwa taifa kama watakuwa tayari ili
watusaidie kubaini majina hayo ambayo siyo yapo Uswisi peke yake bali na
nchi nyingine.”
Alisema
Watanzania waache kupenda mambo rahisi na kwamba, uchunguzi lazima
ufanyike kuwabaini walioficha mabilioni hayo ili fedha hizo zirejeshwe
nchini.Alisema Serikali ya Uswisi haiwezi kuisaidia Tanzania kufanya
uchunguzi wa fedha hizo.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment