Kocha
mkuu wa timu ya Young Africans Sports Club, Mholanzi Ernie Brandts
amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili timu ya Coastal Union katika
mchezo wa mwisho wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom
utakaofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz leo
asubuhi katika mazoezi yaliyofanyika shule ya sekondari Loyola, amesema
wachezaji wake wote wapo safi, wana ari ya mchezo na ushindi, hivyo
anaamini mchezaji yoyote atakayempanga atafanya vizuri.
Wachezaji
wangu wapo fit wote, nadhani soka waliolicheza siku na Azam
lilionekana, hizo ni dalili tosha kuwa wachezaji wanaelewa mafunzo
yangu, hivyo naamin siku ya jumapili vijana wangu wataibuka na ushindi
mzuri hali itakayotupelekea kuweza kuendelea kushika usukani wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara amesema 'Brandts'
Coastal
Union inayoshika nafasi ya nne katika msimo wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania bara, itashuka dimbani siku hiyo ya jumapili kusaka pointi ili
kujiweka katika nafasi ya kuendelea kushika nafasi tatu za juu
Yanga
ambayo mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa mabao 2 - 0 dhidi
ya timu ya Azam FC katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki, itaingia
uwanjani kusaka pointi 3 muhimu zitakazo ifanya iendelee kuongoza
msimamo wa Ligi Kuu kwani kama Yanga ikishinda basi Simba na Azam hata
zikishinda hazitoweza kuongoza Ligi.
Katika
mazoezi yaliyofanyika leo asubuhi, kocha Brandts ameendelea kufurahia
kuwepo kwa wachezaji wake wote, kitu kitakachopelea kumtumia mchezaji
yoyote atakayetaka kumtumia kwa mchezo huo wa jumapili, kwani hakuna
mchezaji aliye majeruhi .
Vijana
wa jangwani kwa sasa wanakamata nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kufikisha point 26, mbele ya Azam
yenye pointi 24 na Simba yenye pointi 23 huku timu zote zikiwa
zimecheza michezo 12.
No comments:
Post a Comment