Taarifa
zilizopatikana jioni ya leo zinaeleza kuwa aliyewahi kuwa muigizaji
katika kikundi cha Kaole,(pichani enzi za uhai wake) ,aliyekuwa
akitambulika kwa jina la Mlopelo amefarika dunia mapema leo hospitali ya
Temeke,jijini Dar,kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu wameitonya
Blog ya Jiachie kuwa Marehemu Mlopelo amefarika mchana wa leo kwenye
hospitali ya Temeke mapema mchana wa leo, na kwamba shughuli zote za
Msiba zipo nyumbani kwao Temeke Wailess mtaa wa Boko,imeelezwa kuwa
mazishi yake yatafanyika mapema kesho saa nne.Wadau Taarifa kamili
tuvute subira kidoogo tutakuja juzana hapa hapa jamvini tena.Mungu
ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amen.
MWENYEKITI WA CCM DKT. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU CCM TAIFA
DODOMA
-
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 17 Januari 2025, ameongoza
Kikao c...
16 hours ago
No comments:
Post a Comment