HABARI
kutoka Chuo Kikuu cha Kampala Tawi la Dar es Salaam Tanzania, zinapasha
kuwa Wahadhiri na wafanyakazi wa Kawaida wa chuo hicho wameingia katika
mgomo kuanzia leo.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi chuoni hapo na kuifikia
meza ya Father Kidevu Blog, wanadai kuwa Wahadhiri hao wameanza mgomo
wao leo wa kutoingia madarasani kufundisha kufuatia madai yao ya
mishahara na posho nyingine.
Wanafunzi
hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao wanasema kuwa walihao walikaa
kikao jana na kufikia muaafaka huo wa kuingia katika mgomo wa kudai
mishara yao na hawatoingia madarasani hadi pale watakapolipwa fedha zao
hizo.
“Awali
tulikuwa tukisikia kuwa wanadai mishara ya miezi mitano yaani tangu
mwezi mei hawajalipwa lakini kwa mujibu wa taarifa zilizo samba chuoni
hapo leo ni kuwa madai ya wahadhiri hao yalioyobaki hadi sasa ni ya
miezi miwili.” Alisema Mwanafunzi huyo.
Wanafunzi
hao walidai kuwa kuwepo kwa mgomo huo kutawaathiri kimasomo kwani wapo
baadhi yao wanaoingia katika kufanya mitihani hivi karibuni na wanafunzi
wa mwaka wa kwanza ndio kwanza wameripoti chuoni hapo hivyo wanahitaji
kupata mafunzo zaidi na si kukutana na migomo hiyo.
No comments:
Post a Comment