Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 13, 2012

NADIR HAROUB "CANNAVARO" NA BAHANUZI WAONDOKA LEO KWENDA KWENYE MAJARIBIO CHINA




 YANGA imethibitisha kwamba straika wake, Said Bahanuzi pamoja na beki Nadir Cannavaro wataondoka leo Jumanne jioni kwenda Shanghai, China kwa majaribio lakini Haruna Niyonzima 'Fabregas' akili yake ipo Ubelgiji. 
Ingawa wachezaji hao walifanya siri, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Abdallah Bin Kleb alithibitisha kwamba wanakwenda kwenye klabu moja ya daraja la pili na watakaa huko wiki mbili na wamewaruhusu kwa kuwa ligi imesimama. 
"Kama wakifuzu tutakaa chini tujadiliane na tujue wanahitajika lini na sisi tutanufaika vipi na wachezaji wenyewe watanufaika vipi kimaisha," alisema Bin Kleb akidai kwamba bado wanahitajika Jangwani lakini Wachina wakipanda dau watawaachia kwa maslahi yao na nchi. 
Haruna kwa upande wake alisema: "Naweza kuondoka wakati wowote kuanzia sasa kwenda Ubelgiji na sasa nasikilizia mpango huo na nafikiri uko katika hatua za mwisho, mipango itakapokamilika nitasubiri ruhusa ya viongozi kwani wao ndiyo wenye uamuzi wa mwisho kwa sababu mimi bado ni mchezaji wa Yanga." 
Akikizungumzia kikosi cha Yanga, Fabregas alisema: "Tusibweteke tujiandae kila mmoja kwa nafasi yake ili tufanye vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara."

No comments:

Post a Comment