Raia mmoja wa Marekani anayesadikika kuwa mfuasi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaed amehukumiwa kifungo cha miaka 17 jela kwa kupanga njama za kushambulia Wizara ya Mambo ya Ulinzi ya Marekani na jengo la bunge la nchi hiyo kwa kutumia mfano wa ndege zilizojazwa mabomu na kuendeshwa kwa kutumia rimoti. 
Mwezi Julai mwaka huu Rezwan Ferdaus mwenye umri wa miaka 27 alikiri mashtaka yanayomkabili ya kupanga njama hizo.
Ferdaus alikamatwa mwaka 2011 baada ya operesheni kali iliyofanywa na Shirika la Ujasusi la Marekani-FBI ya kuwatafuta wafuasi ambao iliamini ni wa mtandao wa Al-Qaeda.
Wizara ya Sheria ya Marekani imeeleza kuwa baada ya kumaliza kifungo hicho cha miaka 17 jela, Ferdaus atakuwa chini ya ulinzi mkali kwa miaka 10.