Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekuwa Mwenyekiti Mpya wa Ukanda wa Kiuchumi wa Nchi za Afrika Mashariki na Kusini (COMESA).
Rais
Museveni amechukua wadhfa huo kutoka kwa rais wa Malawi Joyce Banda
aliyemaliza muda wake, ambaye amekabidhi nafasi hiyo katika Mkutano wa
16 unaoshirikisha wakuu wa nchi na serikali wa COMESA.
Katika
Mkutano huo unaofanyika nchini Uganda na unaotarajiwa kumalizika leo,
Rais Museveni katika hotuba yake amesema uchumi wa nchi za kiafrika
umegawanyika mno, kitu ambacho kinadhoofisha ukuaji wake na kupelekea
nchi hizo kushindwa kuvutia wawekezaji wa kigeni.
Amesema upo umuhimu wa kuwa na umoja wa kibiashara kwa nchi za Afrika.
No comments:
Post a Comment