
HIVI NDIVYO ALIVYOUNGUZWA MTOTO ANETH NA MAMA YAKE MDOGO KABLA YA KUKATWA MKONO JANA

Bahati Rukangara huyu ndiye aliyemchoma mtoto Janeth Mkono wake wa ksuhoto
MTOTO ANETH AKIWA ANAENDELEA VIZURI BAADA YA KUMKATA MKONO WAKE WA KUSHOTO JANA

KWA
UJUMLA MTOTO ANETH SASA ANAENDELEA VIZURI NA ANAKULA CHAKULA VIZURI PIA
TAARIFA TULIZOPATA MUDA SI MREFU MAMA YAKE MZAZI YUPO NJIANI KUJA MBEYA
TOKA KAGERA
ANETH AKUTAYARISHIWA CHAKULA NA MAMA YAKE MDOGO SLIVIA ANAEMUHUDUMIA HOSPITALINI HAPO.Habari naVenance Matinya, Picha na Joseph Mwaisango
--
HALI
ya Mtoto Aneth Johanes (4) aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya kufuatia kuchomwa moto mkono wake wa kushoto na anayedaiwa kuwa
ni Shangazi yake inaendelea vizuri licha ya kufanyiwa upasuaji
uliolazimu kukatwa kwa mkono huo.
Kwa
mujibu wa mama mdogo wa mgonjwa anayemhudumia hospitalini hapo Silvia
Salvatory alithibitisha kuendelea vizuri kwa motto huyo ambapo
alisema ilimlazimu kufanyiwa upasuaji kutokana na mkono huo kukosa
mawasiliano na kuonekana kuvunjika.
Alisema
taarifa za awali zinaonesha shangazi yake huyo Bahati Rukangara
alianza kumtesa mtoto huyo muda mrefu mara baada ya kumchukua kutoka kwa
wazazi wake wanaoishi Bukoba Mkoani Kagera.
Aliongeza
kuwa tangu amchukue kwa wazazi wake Februari Mwaka huu amewahi
kumjeruhi mkono wake wa Kulia hadi kuuvunja ambapo hadi sasa mtoto huyo
alikuwa akitegemea mkono wa kushoto ambao umekatwa.
Tukio
hilo la kisikitisha lilitokea juzi majira ya saa nne asubuhi baada ya
majirani kusikia yowe la mtoto huyo akiomba msaada kutokana na mateso na
maumivu makali aliyokuwa akiyapata kutokana na adhabu hiyo kutoka kwa
Shangazi yake
.
Muuguzi
mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Thomas Isidori alisema hali
iliyopelekea kukatwa kwa mkono wa mtoto huyo ni siri kati yake na
daktari aliyemhudumia na kwamba sheria ya uuguzi inakataza kutoa
taarifa ambazo ni siri.
Isidori
alipoulizwa sababu za mgonjwa huyo kufanyiwa upasuaji mapema mno hadi
kusababisha ulemavu alisema ni suala la kitaalamu ambalo hata yeye
hawezi kulijibu na ni sheria ambayo inawataka madaktari kutunza siri za
wagonjwa.
Hata
hivyo muuguzi huyo alizuia kabisa waandishi wa habari kupiga picha za
motto huyo baada ya kufanyiwa upasuaji huo uliosababisha kukatwa mkono
kwa mgonjwa huyo.
Baadhi
ya wananchi waliofika Hospitalini hapo kumjulia hali mtoto Aneth
aliyelazwa Wodi namba Nane ambao hawakutaka kutaja majina yao walilaani
kitendo cha madaktari kukimbilia kukata mkono mgonjwa badala ya
kujaribu njia zingine za kunusuru hali hiyo.
***KUNA
UTARATIBU MAALUM AMBAO UNAANDALIWA HIVI SASA JINSI YA KUMSAIDIA MTOTO
ANETH KWA MSAADA WOWOTE AMBAO WADAU WETU WATUKUFU MTAKUA TAYARI
KUTOA/KUJITOLEA,ENDELEA KUDURUSU UKURASA HUU KWA UPDATE ZA MARA KWA MARA
ZA HALI YA MTOTO ANETH

huyo mama inabidi afungwe maisha jela hana haki ya kuishi uraiani katika jamii, ana roho ya kinyama.
ReplyDelete