![]() |
| Maganda ya risasi zilizo tumika. |
jiji la Mwanza.
Mtu huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake
ametambuliwa kwa jina moja tu la Greda.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari
wa halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa katika maeneo yao ya
kazi
eneo la barabara ya Pamba kwenye stendi ya zamani ya mabasi ya
Tanganyika karibu na soko kuu la jiji hilo, wakiwa katika operesheni zao
za kawaida za kusafisha jiji walikamata bidhaa zilizokuwa zimepangwa
katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria wakiwa kwenye eneo hilo mtu
mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga alimrukia mgambo wa jiji
shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa nia ya kumdhuru.
Baada ya tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi hewani kuwatawanya wamachinga hao waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.
![]() |
| Mmoja wa viongozi wa akiwatuliza wamachinga wenzake kupata kumsikiliza mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. . |
![]() |
| Maduka mengi hususani yaliyo karibu na eneo la tukio yamefungwa kufuatia seleka hilo. |
![]() |
| Mmoja kati ya viongozi wa wamachinga akizungumza na wenzake kuwasihi kulinda utulivu ili haki yao isipotee. |
![]() |
| Polisi wakiwa kwenye doria eneo la tukio. |










No comments:
Post a Comment