Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo.Picha Na Mbeya Yetu Blog
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf
Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti yake wa kumzaa(15) jina lake
limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi wa binti huyo Bi, Regina Simon(35)
baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu kuwa binti yake ana ujauzito wa
miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa Balozi wa mtaa huo Bwana
Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kitongoji
Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio
hilo,lakini mtuhumiwa alikanusha ingawa binti yake alithibitisha
kutendewa ukatili huo na kwamba alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila
alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa
waliamua kuipeleka kesi hiyo Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha
binti huyo kupelekwa kwa
No comments:
Post a Comment