![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEghOtAvocwrJvj2VUyhDZMTqkjE8zGtN_YpMk-_QfwMZGtkX1zkcLwnrPlZfQbOeUhrUUf4eq8O1j99g_t2Dop12pdxY6HxTaJHqVSBV1_aOifh8X3sLBr-c9b5GRHyIso6fdXcTU3yoIA/s1600/rail;a.jpg)
WAZIRI
wa Ujenzi, Dk John Magufuli jana aliungana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe,
Morgan Tsavangirai kumpigia debe mgombea wa urais wa Kenya, Raila Odinga
huku akisema mgombea huyo kupitia Chama cha Orange Democratic Party
(ODM), anastahili kuwa Rais wa nchi hiyo kutokana na sifa zake za
uongozi.
Akizungumza
katika Mkutano Mkuu wa ODM jana, Dk Magufuli alisema hakuna sababu
zozote zitakazowafanya Wakenya wasimchague Odinga.
“Nataka
kuwaambia Wakenya kwamba Odinga ni mcha Mungu, mnatakiwa kujua hilo.
Kama mimi ningekuwa Mkenya ningempigia huyu jamaa kura ili aongoze nchi.
Lakini sasa kwa kuwa siruhusiwi hata kupiga kura, basi nawaambia
msiache kumchagua huyu atawaongozeni vizuri,” alisema Dk Magufuli.
Dk
Magufuli alisema kati ya wagombea wote waliojitokeza kuwania kiti cha
urais nchini Kenya, hakuna anayemfikia Odinga na hiyo inaonyesha kuwa
wakimchagua atawasaidia bila ubaguzi.
Alisema na hata Odinga ambaye ni Waziri Mkuu wa Kenya akiamua kugombea ubunge katika Jimbo lake la Chato, hawezi kumshinda.
“Kwa
hiyo nasimama hapa ndugu zangu wana ODM kuwapa pongezi kubwa sana,
mmmefanya kitu kikubwa sana kwa sababu mmechagua jembe,” alisema.
Huku
akishangiliwa na maelfu ya wajumbe wa mkutano huo, Dk Magufuli alisema
kama angekuwa akipiga kura angempa Odinga kura zake zote kwa sababu ni
mtu mwenye upendo,
uvumilivu, asiye na makuu wala ubaguzi na anayependa kushirikiana na watu wote.
uvumilivu, asiye na makuu wala ubaguzi na anayependa kushirikiana na watu wote.
Alisema
Odinga ni mpenda amani na kusisitiza kuwa amelisema hilo kwa sababu
amani ni muhimu katika maendeleo ya Afrika Mashariki na Afrika kwa
jumla.
Alikipongeza
chama hicho kwa kuamua kushirikisha vyama zaidi ya 15 na kuweka nguvu
zao pamoja ili kushinda katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika
Machi 4, 2013.
Akizungumzia
uhusiano wake na Odinga, Dk Magufuli alisema walifahamiana tangu
alipokuwa Waziri wa Ujenzi wa Kenya wakati yeye akiwa Waziri wa Ujenzi
wa Tanzania.
“Uliwahi
kufika Tanzania mara nyingi na hata kuhudhuria mazishi ya baba yangu
mpendwa, ukaja na mawaziri zaidi ya watano pamoja na mke wako katika
jimbo langu ninalotoka linaloitwa Chato,” alisema.
Bila
kuwataja majina, aliwapiga vijembe baadhi ya wagombea wengine nchini
Kenya akisema hawawezi kutembea nje ya nchi hiyo kutokana na kubanwa na
sheria, huku akisema Odinga ana uwezo wa kutembea ulimwenguni kote bila
pingamizi.
Kuhusu
Muungano wa vyama vya kisiasa nchini humo, Dk Magufuli alisema hiyo
inaleta changamoto kwa siasa za Kenya… “Huu ni muungano mzuri ambao
naukubali sana, hususan walioungana na Odinga ni dhahiri kabisa kwamba
wanamtabiria ushindi mkubwa.”
Alisema
Wakenya wanatakiwa kuachana na uongozi wa makabila akisema
hautawafikisha popote kwani ni kikwazo cha maendeleo na pia ndicho
chanzo cha migogoro nchini humo.
“Msilete
ukabila… mtakuwa mnaivuruga Kenya yote, watu watakufa, watakosa uhuru
wa kuishi sehemu moja kama Waafrika wengine,” alisema.
Alisema
vurugu zinazofadhiliwa na utawala uliopo madarakani na ukandamizaji wa
washiriki wengine wa shughuli za kisiasa hauhalalishi uchaguzi kuwa huru
na wa haki.
Aliwaonya
wajumbe hao kutorudia tena kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama
ilivyo sasa kwa kuwa Serikali ya aina hiyo hujenga chuki kati ya
viongozi na kudhoofisha utendaji wa Serikali.
“Hakikisheni
mnaipigia kura ODM kwa wingi ili ishinde Uchaguzi Mkuu ujao na kuunda
Serikali moja ambayo itapimwa kwa kuzingatia programu zake.
Naye
Tsavangirai aliwataka Wakenya kuepuka machafuko na wale ambao watakuwa
wameshindwa katika kinyang’anyiro hicho cha urais, wakubali matokeo.
Aliungana na Dk Magufuli kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa akiwataka isiwepo kwa madai kuwa ni chanzo cha migogoro.
“Serikali ya Muungano ni chanzo cha migogoro kwani kila mgogoro uliopo Afrika unasabaishwa na Serikali ya Muungano,” alisema.
No comments:
Post a Comment