MACHINGA
wa Mji wa Moshi leo walileta kizaa zaa katika mji wa Moshi baada ya
Wafanya biashara hao wadogo kufunga barabara ya Ghala, wakipinga
kitendo cha Uongozi wa Manispaa ya Moshi, kuvunja Gereji ya Bantu,
wanayoitumia kama sehemu ya kuhifadhia bidhaa zao.
Akizungumza
na Machinga hao katika juhudi ya kuhakikisha usalama unarejea kama
kawaida, RCO Nga’azi aliwataka viongozi wa Wamachinga kuwatuliza wafuasi
wao, nakuangalia njia nyingine ya kutafuta haki kwa amani.
Alisema
kuna umuhimu wa kila mwananchi kutambua wajibu wa kudumisha amani na
kuwakumbusha umuhimu wa kuhakikisha haki wanayoitafuta haikiuki haki za
binadamu na Raia wengine wa nchi hii.
Akizungumza
na wamachinga hao, muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la tukio,
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi, aliwaahidi wachinga hao
kufanyia kazi tatizo lao na kuwaomba wateue wawaklishi wao wanne ambao
aliandamana nao hadi katika ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi,
Bernadeta Kinabo, kuzungumza Tatizo na kulipatia ufumbuzi.
“Nimesikia
tatizo lenu na kilio chenu ndio maana niko hapa, nataka niwahakikishie
kwamba le oleo mtapata majibu kutoka kwangu, kwa sasa ninachowaomba nim
kila mtu arejee katika shughuli zake za kawaida ili amani ya mji wetu
uendele kuwepo,” alisema Msengi.
Kwa
upande wao, baadhi ya Machinga wanaodaiwa kuvunjiwa na kuharibiwa mali
zao katika tukio hilo lililotokea jana , majira ya saa saba usiku,
Abdallah Abushehe na Mwamedi Ally, walisema kuwa, asubuhi ya leo
waliamka na kufika katika gereji hiyo wanayo itumia kuhifadhia bidhaa
zao na kukuta eneo hilo limevunjwa na baadhi ya mali zao kupotea.
“Mimi ni
fundi viatu, kawaida yetu ni kuhifadhi bidhaa zetu hapa gereji,
wamevunja usiku usiku hata taarifa hawajatupa, hawa wagambo wamezidi
kutuonea sana, kila siku wanatukimbiza wanatunyima raha kweli ya kufanya
kazi, sasa hivi mkokoteniwangu na magunia yangu ya viatu siyaoni, kwa
kweli sisi tumechoshwa na uongozi wa Manispaa,” alisema Ally.
Naye
mmiliki wa Gereji ya Bantu lililovunjwa na kuzaa mzozo huo, Abdillahi
Ally, alikiri kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa mji wa Moshi,
Bernadetta Kinabo kuhusu eneo hilo kuwepo katika ramani za ujenzi wa
Nyumba za shirika a Nyumba Taifa (NHC).
Alisema
kuwa aliwahi kupata Barua kutoka kwa Meneja wa NHC, iliyosainiwa na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, ikimtaka kuachia sehemu hiyo ndani ya
siku mbili, lakini kutokana na kutoridhika na maamuzi ya hayo alifungua
kesi Mahakamani.
No comments:
Post a Comment