WAZIRI wa
Ujenzi, John Magufuli amemteua Prof Ninatubu Lema kutoka Chuo cha
Uhandisi na Teknolojia (CoET), kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa
Wahandisi (ERB), uteuzi huo unaanzia Desemba 20 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa taarifa ya Magufuli iliyosambazwa kweye vyombo vya habari
jijini Dar es Salaam jana, na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi
Herbet Mrango, ilieleza kuwa uteuzi huo, utadumu kwa kipindi cha miaka
mitatu hadi Desemba 20, 2015.
Kwa
mujibu wa sheria Na. 15 ya mwaka 1997 ya mabadiliko madogo ya sehemu ya
3(3) ya kifungu 1(1) (a), na 1(2), kama ilivyorekebishwa na Sheria Na.
24 ya mwaka 2007, ndiyo iliyomfanya Waziri afanye uteuzi wa wajumbe wa
Bodi hiyo akiwemo mwenyekiti huyo.
Katika
uteuzi huo, Magufuli pia aliwataja wajumbe wanane wa bodi hiyo ya ERB,
kuwa ni pamoja na Fintan Kilowoko kutoka wizara hiyo, ambapo kwa sasa ni
mkurugenzi wa Barabara za Mikoa, Joseph Malongo, ambaye kwa sasa ni
Msajili Msaidizi Huduma za Usajili na Gemma Modu kutoka Baraza la taifa
la Elimu ya Ufundi (NACTE), Nuberis Nyange kutoka Chama cha Wahandisi
Washauri nchini (ACET).
Wengine
ni Sarah Barahamoka, kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Edwin
Ngonyani kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Prof Bakari Mwinyiwiwa;
Mhandisi Mwandamizi, Chuo cha Uhandisi na Teknolojia (CoET), kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es salaam na Prof. John Kandoro; Mkuu wa Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam (DIT).
Waziri
alisema kuwa jukumu la msingi la Bodi hiyo ya Usajili wa Wahandisi ni
kusajili wahandisi pamoja na Kampuni zinazotoa ushauri wa kihandisi,
kuendeleza wahandisi kitaaluma, kuwajengea uwezo wa Wahandisi wa
kitanzania.
Pamoja na kuandaa nakuchapisha makala mbalimbali yanayohusu shughuli za kihandisi nchini.
No comments:
Post a Comment