Baada ya kusumbua kwa muda mrefu na ngoma yao ya Mbeya nyumbani, Wasanii wakali kutoka jijini Mbeya hapa nawazungumziaMbeya All Stars wanakuja na pini jipyaaaaaaa linalokwenda kwa jina laSalam toka Mbeya. Akiongea na mhariri wa UJIO WANGU vice president wa Mbeya All Stars Doctor Fazi amesema "Ngoma hiyo inatarajiwa kuachiwa rasmi kesho tar 13/12/2012"
Akizungumzia ngoma hiyo producer wa ngoma hiyo Zest Mkali kutoka Moja
Moja records amesema kwamba kutakua na wasanii wapya ambao
hawakushiriki kwenye nyimbo zilizopita hii ni kuonyesha kuwa dhamira ya
Mbeya All Stars ni kuinua vipaji na kuvitangaza kuanzia nyumbani.
Pia vice president wa Mbeya All Stars ameongeza kua hivi karibuni kutakua na ujio wa blog mpya itakayoitwa THE GREEN CITY PROFILEitakayokua ikizungumzia ma-celebrity wa jiji la Mbeya kwa kuweka picha zao na CV zao.
Stay tuned mambo mazuri Kutoka MBEYA ALL STARS yanakuja.
No comments:
Post a Comment