Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kuona taarifa ya mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa JWTZ wa Kambi ya Monduli, Arusha, iliyochapishwa katika
Baada ya kuona habari hii JWTZ linafanya uchunguzi wa kina ili kutambua kama mtu huyo ni askariwa kweli au la. Kimsingi, JWTZ linafanya uchunguzi wa kumtambua mtu huyo kama kweli ni askari wake kwa sababu zifuatazo; kwanza Jina la mtu huyo halijaandikwa, pili kikosi halisi cha mtu huyo hakijaandikwa kwani eneo la Monduli lina vikosi vingi na hakuna kikosi kiitwacho Monduli. Lakini pia inatia shaka kuwa mavazi yale siyo yale yanayotumika kwa wanajeshi wa JWTZ hivi sasa, kuna tofauti kati ya jampa(jacket) na suruali kama ilivyooneshwa katika picha hiyo. Aidha, jampa la sare hiyo pia lina tofauti katika sehemu za mikono, jambo ambalo linatia shaka kamani sare halisi ya JWTZ.
Ilikuwa rahisikumtambua mtu huyo kwa kuangalia uso, lakini mtu huyo anayedaiwa kuwa ni askari alifunika paji la uso ili asitambulike. Pamoja na hali hiyo ilivyojitokeza, JWTZ linashughulika kumtambua mtu huyo kwa kutumia mbinu mbalimbali. JWTZ litakapobaini ukweli huo, hatua za kinidhamu zitachukuliwa kutokana na Kanuni za Majeshi ya Ulinzi kwani, Sheria nambari nne (4) ya mabadiliko ya nane (8) katika Katiba ya Nchi ya mwaka 1992 ibara ya 147(3), mwanajeshi yeyote hatakiwikujihusisha katika masuala ya kisiasa.
Kama ilivyoelezwa hapo juu, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa kuchapishwa kwa picha hiyo kwani hakuna tija wala faida kwa wananchi wa Tanzania zaidi ya kuwatia hofu kuwa Vyombo vya Ulinzi navyo vinashabikia mambo ya siasa, wakati Katiba ya nchi imekataza jambo hilo. JWTZ linawaomba wananchi waliangalie jambo hili kwa makini, kwa usalama wa nchi yetu.
Imetolewana Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga
MakaoMakuu ya Jeshi, Upanga
source:http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/373747-tamko-la-jwtz-juu-ya-picha-ya-lema-na-mwanajeshi-katika-mwananchi-la-leo.html
No comments:
Post a Comment