Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 13, 2014

UNALIJUA KABILA LA WAKINGA?SOMA HISTORIA YAO HAPA............

Wakinga ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Iringa, Wilaya ya Makete. Lugha yao ni Kikinga.Asili ya lugha hii ni Misitu ya Kongo  Makabila makubwa mkoani Iringa ni Wahehe, Wabena,Wakinga na Wapangwa. Kabila la Kihehe ndilo kubwa kupita makabila mengine. Asilimia ipatayo 43 ya idadi ya watu wote Mkoani ni Wahehe. Watu wa kabila hili wanaishi wilaya za Iringa na Mufindi - kabila linalofuata kwa ukubwa ni Wabena ambao ni asilimia 37 ya wakazi wa Mkoa huu, Wakinga ni asilimia 11 na Wapangwa asilimia 3. Kabila la Kibena liko wilaya ya Njombe na eneo la Malangali likiwa linapakana na wilaya ya Ulanga na Kilombero (Mkoa wa Morogoro). Wakinga wako wilaya ya Makete na Wapangwa wako eneo la Malangali. Yapo pia makabila madogo kama vile Wakisi, Wamanda n.k ambao kwa ujumla wao wanachukua asilimia 6 iliyosalia ya watu Mkoani Iringa. Kwenye Maendeleo utaona Iringa matajiri na wenye nyumba nzuri ni wabena na wakinga ambao ni wachapa kazi sana tofauti na wahehe.Tanzania nzima mkoloni aligundua makabila maatatu kuwa ndio wachapa kazi za mikono na wenye kujituma na waaminifu kazini kuliko makabila yote.

Makabila haya ni
1.Wabena toka njombe,Iringa 2.Wakinga toka makete,Iringa 3.Waha toka kigoma 
BARABARA Wilaya ya Makete ambayo inategemea barabara mbili kuu ya kutoka Njombe na nyingine kutoka Mbeya, kipindi hiki moja ya kutoka Njombe inapitika, lakini barabara pacha zinazoingia mkoani Mbeya zimeharibika na haipitiki.
Ubovu wa barabara hizo, umechangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha usafirishaji wa pembejeo na hivyo hazifiki kwa wakati.
Lakini pia umechangia kushindwa usafirishaji mazao kama matunda, viazi, pareto, mazao ya mbao, ngano, mahindi na mengine kwenda sokoni. Barabara wilayani humo kama katika wilaya nyingine kama zinapitika, zinachangia kukuza uchumi wa wilaya hiyo, lakini zinazopokuwa mbovu zinachangia kupunguza kasi ya kukua kwa uchumi, pato la wananchi na maendeleo wilaya hiyo.
Ubovu wa barabara wilayani humo, umepandisha bei ya bidhaa za madukani ambazo zinaingizwa wilayani humo kupitia Mbeya na Njombe. Bei ya bidhaa nyingi hasa katika maeneo ambayo barabara zimeharibika, bei zake ni za kuruka.

Kutokana na ubovu wa barabara hizo, wananchi wa maeneo ya Bulongwa, wanabeba matunda, ngano na bidhaa nyingine kwa kichwa umbali mrefu kwenda kuuza mkoani Mbeya ambako soko linapatikana.
Adha ya ubovu wa barabara, zimewakumba pia wakazi wa Ipepele, Iniho na Matamba wilayani humo, wamekuwa wakibeba viazi, mbao na mahindi vichwani umbali mrefu kwenda kufikisha kwenye maeneo ambako barabara zinafikika.
Kutokana na ubovu wa barabara, mazao mengi ya wilaya ya Makete, yakiwamo ya mbao yamekuwa yakikwama kusafirishwa na hivyo kukwamisha ukuaji wa uchumi wilayani na hivyo kuwakosesha wananchi kipato, ajira na mahitaji ya kila siku. Pareto imekuwa ikisuasua kusafirishwa, hata kama hivi karibuni imefufuliwa baada ya miaka takribani kumi kufifia na wakulima kukata tamaa kutokana na soko la dunia la bidhaa hiyo kuanguka mwanguko wa mende.
Kufufuliwa kwa soko la zao hilo na kuanzishwa kwa malipo ya papo kwa hapo, kumechangia kuamsha ari ya wananchi kulima kwa wingi zao hilo, hata kama ubovu wa barabara unalazimisha baadhi ya mazao kuozea nyumbani.
 TUNAOMBA BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGI MOTOMOTO(USIPITWEEEE)

Mahindi, ngano, shayiri na matunda ambayo yanalimwa kwa wingi Bulongwa na Matamba, yanaozea mitini. Watu wachache wenye uwezo wanabeba kichwani umbali mrefu kwenda kuuza. Wenyeji pia wanazao la miti ya ulanzi linalotoa ulanzi  Wenyeji wa wilaya hiyo, Wakinga, ni wafanyabiashara maarufu katika mikoa mbalimbali nchini hasa Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, Ruvuma na Rukwa na maeneo mengine. Lakini, wamekuwa wakishindwa kuwekeza wilayani kwao kutokana na barabara nyingi kuwa mbovu na kutopitika wakati wote.
Kama serikali imedhamiria kuikomboa wilaya ya Makete, barabara ndio chanzo za maendeleo. Inatakiwa zijengwe kwa kiwango cha lami. Zikijengwa kwa lami, zitasaidia kuongeza haraka pato la wananchi, kukuza uchumi wa nchi na kuondoa umasikini wa wana-Makete

No comments:

Post a Comment