Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, December 6, 2012

STARS,HEROES LAZIMA KIELEWEKE LEO



 Kikosi cha Kilimanjaro Stars.Picha na Bongo Staz

 Kikosi cha Zanzibar Heroes.

KILIMANJARO Stars na Zanzibar Heroes, leo zinaweza kuandika 
historia ya kupeperusha bendera moja ya Tanzania kwa kucheza fainali
 ya Kombe la Chalenji, lakini hilo linawezekana iwapo tu zitashinda 
mechi zao za nusu fainali leo hii kwenye Uwanja wa Namboole.

Stars itaikabili Uganda, wenyeji wa michuano hiyo katika nusu 
fainali ya pili, huku Heroes ikipepetana na Kenya katika mchezo 
mwingine wa hatua kama hiyo utakaoanza mapema.
Stars na Heroes mara ya mwisho zilikutana hatua ya makundi 
nchini Malawi, na Bara kulala kwa bao 1-0 na hivyo kukosa 
nafasi ya kusonga mbele wakati Zanzibar haikuwa na la kupoteza
 kwenye mchezo huo.

Timu hizo pia zinaweza kukutana zenyewe katika hatua ya kuwania
 nafasi ya tatu, iwapo zote zitapoteza mechi zao mbele ya Kenya 
na Uganda inayopewa matumaini makubwa ya kutetea taji.

Hata hivyo, dhamira ya kila upande ni kushinda mechi hizo na 
kucheza hatua ya fainali ili kutwaa taji pamoja na kitita cha pesa 
kutoka kwa wadhamini wa michuano hiyo, kampuni ya kutengeneza
 bia aina ya Tusker.

Mtazamo wa kiupinzani unatarajia kuonekana kwenye mechi 
zote zinazozikutanisha timu kutoka nchi waanzilishi wa Jumuiya 
ya Afrika Mashariki, huku mchezo kati ya Uganda na Tanzania 
ukionekana kuwa kiini cha ushindani.

Stars yenye kujiamini na kujivunia kiwango kizuri kuwahi 
kushuhudiwa usoni mwa mwashabiki wa soka miaka ya
 karibuni, itakuwa na kazi ya kulipa kisasi cha mabao 3-1 
walichopata kutoka Uganda kwenye michuano iliyotangulia jijini
 Dar es Salaam.
Kocha wa Stars Kim Poulsen anatarajiwa kuwapanga viungo wake 
mahiri
Mwinyi Kazimoto na Salum Abubakar ili kuzima mipango ya 
The Cranes, ambayo hakuna shaka itaratibiwa na Geofrey Kizito na
 Hassani Waswa.

Ili kuwadhibiti washambuliaji matata wa Uganda chini ya Brian 
Umony, Kim atampanga Kelvin Yondan kucheza beki ya kati a
kisaidiana na Shomari Kapombe na pembeni watakuwa Amir 
Maftah na Erasto Nyoni.

Katika ushambuliaji, Kim ataendelea kuwatumia John 
Bocco na Mrisho Ngassa wanaoongoza kwa pamoja orodha 
ya wapachikaji mabao ili kuhakikisha nyavu za The Cranes
 zinakuwa hatarini ingawa watasaidiwa kwa karibu na Amri 
Kihemba pamoja na Frank Domayo.
Akizungumzia mchezo huo, Kim alisema kuwa kikosi chake
 kipo katika hali nzuri kimwili na kiakili kuweza kuikabili 
The Cranes na kupata matokeo mazuri.

Kwa upande mwingi, Kocha wa Heroes alisema kuwa kikosi chake
 kina morali ya hali ya juu kushinda mchezo dhidi ya Kenya.
 
Chanzo:Mwananchi.

No comments:

Post a Comment