Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.
Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.
Mmoja wa
walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na
wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake
wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao
kuungwa mkono na wazazi wao.
Akizungumza
kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye
wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake
hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.
“Tumevumilia
vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu
wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine
hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono)
watoto wao,” alieleza.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.
Mwalimu huyo alidai kuwa walimu: http://www.mwananchi.co.tz/
No comments:
Post a Comment