MKALI
wa filamu hapa nchini, Steve Nyerere amedaiwa kushika nafasi ya kwanza
kwa wasanii wanaowaunganisha na mapedeshee warembo wanaofanikiwa katika
game la filamu Bongo.
Kutajwa
huko kumekuja wakati ambapo kashfa hiyo imezidi kushika nafasi katika
sanaa, huku wadau wakisema Steve Nyerere ni kiboko kwa kuwaunganisha na
watu wasanii wa kike.
Habari
kutoka kwa mtu wa karibu na msanii zinasema kwamba mkali huyo mwenye
manjonjo mengi, alisema watu hao wamekuwa wakipitia zaidi kwa jamaa huyo
ili wawanase warembo.
Alisema
jambo hilo linamuweka katika mazingira magumu msanii huyo, ambaye
anajulikana pia kwa uwezo wake kuigiza sauti za watu maarufu, akiwamo
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
"Yule
jamaa anajulikana kwa kazi hiyo, lakini sidhani kama ina ukweli hasa
ukizingatia kwamba baadhi yao wanasema hivyo wakiangalia ukaribu wa
msanii huyo na wasanii wa kike.
"Kwa
mfano watu kutoka mikoani wenye uwezo mkubwa kifedha, wanadaiwa kuwa
wakitaka ukaribu wa aina yoyote na wasanii wa kike wa Tanzania wenye
majina hupitia kwake,” alisema mpashaji huyo ambaye naye alitembelea
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, wasanii hao wa Bongo Movie
walipofanya ziara.
Kule
mikoani, Steve Nyerere ndio alikuwa kinara wa kushika kipaza sauti na
kuwaita wasanii waliokuwapo kwenye msafara huo wa Fiesta 2012,
akiwawataka pia wacheze jukwaani.
No comments:
Post a Comment