Kikosi
cha timu ya Chama Cha waandishi wa habari za Mizhezo TASWA FC kikiwa
katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kirafiki kati
yake na timu ya Bagamoyo Veteran uliofanyika kwenye uwanja wa
Mawanakerenge Mjini Bagamoyo jioni ya leo, ambapo timu ya TASWA FC
imechapwa magoli 4-0 na maveterani hao kutoka mjini Bagamoyo,
Timu ya Waandishi wa habari ya
TASWA FC imeshiriki katika mchezo huo ikiwa ni moja ya programu ya
mkutano wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika kesho kwenye hoteli ya
Kiromo View mjini Bagamoyo ambapo utafunguliwa na Ridhiwani Kikwete na
Kufungwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndugu Assah Mwambene.
Hiki ndiyo kikosi cha timu ya Bagamoyo Veteran kilichotoa kichapo kwa timu ya TASWA FC mjini Bagamoyo leo.(jana)
Baadhi ya waandishi wa habari ambao ni mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mjumbe
wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba Ibrahim Masoud katikati
akizungumza na Mzee Willy Chiwango kutoka gazeti la This Day kulia na
Beny Kisaka mkurugenzi mwanadamizi gazeti la Jambo Leo.
No comments:
Post a Comment