Na: Boniface Meena
JESHI la Polisi nchini limeibuka na kusema linamsubiri Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka kufika polisi na kutoa taarifa yake rasmi kuhusu tukio lililomtokea Juni 26, mwaka huu.
JESHI la Polisi nchini limeibuka na kusema linamsubiri Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka kufika polisi na kutoa taarifa yake rasmi kuhusu tukio lililomtokea Juni 26, mwaka huu.
Akizungumza
na Mwananchi jana, msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema kuwa,
wanamsubiri Dk Ulimboka afike polisi na kutoa taarifa yake rasmi pamoja
na ushirikiano ili wapate kujua nini kilichotokea.
“Wakati
ule hatukumhoji kwa kuwa alikuwa anaumwa tokea hapo, hatujapata taarifa
yake hivyo, sisi tunamsubiri aje kutoa taarifa yake na atupe ushirikiano
katika suala hilo,” alisema Senso na kuongeza:“Tunataka kujua hali
yake, lakini sisi tunamsubiri aje ili tupate ushirikiano wake.”
Kabla ya polisi kutoa taarifa hiyo jana, Oktoba 28, mwaka huu, Dk Ulimboka aliibuka na kusema yuko imara na anajiaanda kuanika waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Dk
Ulimboka alisema kuwa kamwe hajanunuliwa na kuwa kwake kimya kwa muda
mrefu kumetokana na kufuatilia kwa karibu masharti ya matibabu yake na
si vinginevyo.
“Sijanunuliwa,
sijawaogopa watesi wangu, wala sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata
hao wanaoeneza taarifa kuwa nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa
kuninunua. Bali kimya changu kimetokana na kufuata masharti ya daktari
wangu,” ameeleza Dk Ulimboka kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana
na kununuliwa.
Dk
Ulimboka alikiri kuwa amewahi kusikia taarifa za yeye kununuliwa na
kwamba huwa anajisikia vibaya anapoona kuna kundi la watu linahaha
kutaka kupotosha ukweli na kuchafua jina lake.
“Huo ni
uzushi mtupu. Hata walionitesa wanajua kuwa hawawezi kuninyamazisha au
kuninunua. Wanajua sina bei katika kutetea masilahi ya Umma. Ndiyo maana
wakaamua kutumia njia ile ya kinyama kutaka kunitoa roho yangu.
Siwaogopi wanaodhuru mwili bali yule awezaye kutoa roho. Nakuhakikishia,
muda si mrefu nitaanika kila kitu juu ya kutekwa kwangu, kuteswa na
kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande,” ameeleza.
Juni 26,
2012, Dk Ulimboka alitekwa kuteswa kusukumizwa kwenye gari, kupigwa,
kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye
kutupwa katika msitu wa Mabwepande.
Mwenyekiti
huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania , aliokolewa asubuhi yake na
wasamaria wema karibu na msitu huo, Bunju nje kidogo ya Dar es Salaam.
Akizungumza
kwa sauti ya kujiamini, Dk Ulimboka, ambaye bado hajahojiwa na polisi
wa Tanzania juu ya aliowataja, amesisitiza kuwa alipokamatwa alikuwa na
akili timamu na kwamba waliopanga mkakati wa kumteka anawafahamu.
No comments:
Post a Comment