Ofisa
Masoko wa Kampuni ya Tigo Bw.Alex Msigara.(kulia)Akiongea na waandishi
wa habari (hawapo pichani) leo kwenye Hotel ya Southen Sun jijini Dar es
salaam juu ya kudhamini maadhimisho ya miaka 15 ya bendi ya muziki ya
FM Academia,Sherehe hiyo itafanyika tarehe 14 Desemba mwaka huu msasani
Beach Club ,Ambapo amesema wao kama Tigo wameamua kufunga mwaka kwa
kusaidia jamii wanayoihudumia katika Nyanja zote ikiwemo ya burudani
kama sehemu ya shughuli zao za kijamii .
Amesema
Tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno kwa wateja wote wa jiji la Dar es
salaam kuwapa taarifa kuhusu maadhimisho hayo ya miaka ya 15 ya bendi ya
FM Academia.(katikati)Mwimbaji wa bendi hiyo Bw.Nyoshi El
Sadaat.(kushoto)mratibu wa onesho hilo Bw.Nasibu Mahinya.
No comments:
Post a Comment