Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, December 5, 2012

UTAFITI:SIMU ZA MKONONI HUSABABISHA WATOTO KUZALIWA WATUKUTU.




Kwa ufupi
PIA UHARIBU MIMBA, HUATHIRI NGUVU ZA KIUME NA KUPOTEZA KUMBUKUMBU

mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, 
kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu.

Pia umeeleza kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa
 ubongo na upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao.

Hata hivyo, utafiti huo uliofanywa na Shule ya Tiba na Dawa ya Chuo Kikuu 
cha Yale, Marekani na kuripotiwa na Gazeti la The Telegraph la Uingereza, 
umepingwa na watafiti wengine, wakisema haujakidhi baadhi ya vigezo ili kuuthibitisha.
Kiongozi wa jopo la utafiti huo, Profesa Hugh Taylor alisema utafiti huo 
ulioanzia kwa panya, baadaye ulithibitika kwa binadamu.

Profesa Taylor ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uzazi, Magonjwa ya 
Wanawake na Sayansi ya Uzazi, alisema: “Tulikuwa na panya wenye
 mimba katika maboksi na tuliwawekea simu juu ya vichwa vyao. Panya 
tuliokuwa tumewaweka katika bwawa lile, nusu yao walikuwa wazima na 
nusu yao walikufa. Panya waliokuwa hai tuliwaacha wajifungue na baada 
kujifungua, tukaanza kutafiti watoto wao.”
“Panya ambao hawakuwa karibu na simu za mikononi walionekana kuwa 
. Kumbukumbu zao hazikupungua ikilinganishwa na panya walioathiriwa
 na mionzi ya simu za mikononi ambao katika vipimo vya awali wakiwa 
tumboni, walionekana kuhangaika.”

“Panya hao wenye mimba waliowekwa kwa siku 17 katika boksi hilo na simu 
kupigwa mfululizo juu ya vichwa vyao, walizaa watoto watukutu na 
waliokosa kumbukumbu.”
Aliongeza: “Matokeo hayo yanaweza kutokea kwa binadamu pia. 
anayetumia simu ya mkononi muda mwingi, anaweza pia kuzaa taahira.”

Utafiti huo umebaini kuwa kati ya asilimia tatu na saba ya watoto wenye 
umri wa kwenda shule, wana tatizo la utukutu linaloweza pia kuathiri 
yao kitaaluma. Alisema kiwango hicho kimekuwa kikiongezeka kwa asilimia
 tatu kila mwaka tangu mwaka 1997.

Profesa Taylor alisema anaamini kuwa simu za mikononi pia ni sababu ya
baadhi ya watoto kukosa adabu na pengine kutokuwa makini katika mambo
 mbalimbali wanapokuwa watu wazima.

“‘Huu ni utafiti wa kwanza unaoonyesha ushahidi wa madhara ya
 mionzi ya simu za mkononi. Tumeonyesha kuwa matatizo ya tabia katika
 panya yalitokana na mionzi ya simu za mkononi waliyoipata wakiwa
 tumboni,” alisema Profesa Taylor na kuongeza:

“Kuongezeka kwa utovu wa nidhamu kwa watoto kunaweza kuwa 
sehemu ya madhara ya mionzi ya simu, ambazo mama zao walikuwa 
wakizitumia wakati wao wakiwa bado tumboni.”

Profesa Taylor alifanya utafiti huo kwa kuwachukua panya 33 wenye
 mimba na kuwaweka kwenye boksi lenye nyavu kisha kuweka simu 
juu yake. Simu hiyo ilikuwa ikiita mfululizo kwa siku 17.
Pia aliwaweka panya wengine 33 katika mazingira ya aina hiyo lakini
 hakuweka simu juu ya boksi hilo.
“Zaidi ya watu 160 waliofanyiwa utafiti wa aina hiyo pia walionekana
 kuwa na tofauti za kitabia ambayo inaweza kuhusishwa na utafiti huo.

Hata hivyo, Profesa Taylor alisema kuna haja ya kuendelea kufanya 
utafiti zaidi ili kubaini sababu ya mionzi hiyo ya simu kuathiri watoto 
walio tumboni mwa mama zao na namna bora ya matumizi ya simu 
kwa wanawake wajawazito.

Mtaalamu huyo anatarajia kuungana na wenzake akiwamo Dk Devra 
Davis, anayeongoza Shirika lisilo la Kiserikali la Mazingira na Afya la 
“Environmental Health Trust” kwa ajili ya utafiti zaidi kuhusu madhara ya simu.

Mwaka 2011, Shirika la Kimataifa la Afya Duniani linalojihusisha na
 uchunguzi wa kansa, lilidai kuwa mionzi ya simu inaweza kusababisha

 kansa na hivyo jopo hilo la madaktari linaendelea na utafiti zaidi.

Nchi nyingine duniani ikiwamo Ufaransa, ilipiga marufuku kwa kampuni 
za matangazo ya simu kwa watoto kutokana na hatari mbalimbali
 zinazoweza kuwatokea.

Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la ‘Scientific Reports’ wiki iliyopita
Lengo la utafiti
Ongezeko la matatizo ya magonjwa wa mishipa ya fahamu, matatizo 
mbalimbali ya ubongo pamoja na magonjwa ya akili, ni mojawapo ya mambo
 yaliyochagiza kufanyika kwa utafiti huo.
Dk Hugh alisema simu za mkononi hazina madhara kwa watu wazima kama
 inavyodaiwa na wengi, lakini ni vifaa vyenye kuleta athari kubwa kwa watoto 
tumboni.

“Matatizo yanayowapata watoto wa binadamu walio wengi hivi sasa
 ikiwa ni pamoja na magonjwa ya mtindio wa ubongo, mishipa ya fahamu 
inasababishwa na matumizi ya simu za mkononi kwa mama wajawazito 
na kukaa nazo jirani kwa muda mrefu.”

“Haijalishi mama anaongea na simu au la! Mionzi inapenya na kuleta 
madhara pia kusababisha kazi ya ukuaji wa mtoto katika ubongo
 kulegalega, wapo ambao wanalala na simu kitandani zikiwa zimewashwa..
. hii ni hatari zaidi labda iwe imezimwa,” anasema Dk Hugh.

Watalaamu Dar
Akizungumzia utafiti huo jana, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Nyuklia
 wa Taasisi ya Mionzi Tanzania (Taec), alisema ni vigumu kuukosoa 
utafiti huo kwa sasa hadi hapo Shirika la Afya Duniani (WHO), 
litakapotoa tamko sahihi ingawa alisema mionzi ina athari kubwa kwa binadamu.

“Nilipata kusoma utafiti huo katika mitandao siku mbili zilizopita,
 ni utafiti ambao umewekwa wazi, kwa kweli hata mimi ulinishtua,
 lakini ni mapema kuzungumzia hilo kwa sasa. Kwani utafiti huo bado
 unakinzana kwa mambo mengi, licha ya kupingwa pia na baadhi ya wanasayansi.

“Nadhani ni muda mwafaka sasa kufanya uchunguzi kwa binadamu na 
si kutumia panya kama walivyofanya Chuo Kikuu cha Yale. Hata hivyo,
 jopo la madaktari pia wanatarajia kufanya kikao chao mapema wiki hii, 
labda tutapata maoni mapya.”

Alisema kwa kawaida mionzi ina madhara kwa binadamu, lakini bado
kuna maswali mengi kwa wanasayansi duniani ambayo bado hayajapatiwa
 ufumbuzi, hivyo inawawia vigumu Taec kutoa ufafanuzi wowote kuhusu athari hizo.

Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Innocent Mungy alisema utafiti huo unaweza kuwa msaada mkubwa
 kwa nchi kama Tanzania ambayo hivi sasa ndiyo imechipukia katika 
matumizi ya simu za mkononi. 

Chanzo:www.mwananchi.co.tz  

No comments:

Post a Comment