Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 12, 2013

ANGALIA PICHA NAMNA SHEREHE ZA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YANAVYOENDA KATIKA UWANJA WA AMANI ZANZIBAR!



Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakipita kwa ukakamavu mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein kutoa heshima kwake na Viongozi wa Juu wa Kiserikali waliohudhuria Maadhimisho ya siku ya mapinduzi Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua Gwaride wakati wa Sherehe za Mapinduzi, zilizofanyika leo kwenye Uwanja wa Amani  jini Zanzibar
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Salmin Amour Juma,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
zilizofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho  Kikwete,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume,alipowasili katika Uwanja wa Amaan katika Kilele cha Sherehe za Miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Salmin Amour, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Ameir Pandu Kificho, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu,  Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria katka sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.


Msanii Halikuniki akiongoza Kikundi cha wasanii cha Cha Beni Maarufu(Mbwakachoka) kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium  jini Zanzibar
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.
 Kikundi cha wasanii cha Mbwakachoka kikipita mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakipita kwa Maandamano mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi DK.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) katika sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment