Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea |
Demba Ba akishangilia goli lake katika mechi yake ya kwanza tangu ajiunge na Chelsea |
Nimekuja kufanya kazi... |
Nataka msahau machungu ya kumkosa Drogba |
Ba akishangilia |
Ba akitupia goli la pili |
Hamkukosea kunisajili... Ba akishangilia |
Balotelli akishuhudia mechi yao dhidi ya Watford kutokea benchi leo. |
MSHAMBULIAJI
mpya wa Chelsea, Demba Ba aliyejiunga jana akitokea Newcastle, ameanza
mechi yake ya kwanza na magoli mawili wakati alipoiongoza Chelsea
kushinda 5-1 dhidi ya Southampton katika mechi yaoya Kombe la FA
iliyochezwa leo. Mabingwa watetezi licha ya kutawala mechi, walijikuta wakitanguliwa kwa goli la dakika ya 22 lililofungwa na Jay Rodriguez aliyepachika bao lake la tano msimu huu kufuatia pasi kali ya kupenyezewa na Jason Puncheon. Msenegal huyo aliyekuwa amevaa jezi ya Chelsea kwa mara ya kwanza, aliisawazishia timu yake mpya katika dakika ya 35 akimalizia kuuvusha kwenye mstari mpira ulipigwa na Juam Mata ambao ungeweza kuokolewa na beki wa wenyeji. Muafrika mwenzake Ba, Victor Moses, raia wa Nigeria, aliifungia Chelsea goli la kuongoza katika dakika ya 45 akipiga shuti zuri la mguu wa kushoto kutokea nje ya boksi kufuatia pasi ya nahodha wa kipindi cha kwanza, Ashley Cole. Beki Branislav Ivanovic aliongeza la tatu katika dakika ya 52, Ba akakamilisha mwanzo wake mzuri kwa kufunga la nne katika dakika ya 61 kabla ya Frank Lampard aliyeingia kutokea benchi kufunga la tano kwa penalti katika dakika ya 83. Katika mechi nyingine za leo, Man City ambayo ilimuanzisha benchi mshambuliaji mtata Mario Balotelli kabla ya kuingia katika dakika ya 70 kuchukua nafasi ya Edin Dzeko, iliilaza Watford kwa magoli 3-0 yaliyofungwa na Carlos Tevez kwa 'fri-kiki' ya hatari kutoka umbali wa yadi 25 katika dakika ya 25, Gareth Barry (dk. 44) na Marcos Lopes (dk. 90+1). Tottenham ilishinda kwa magoli 3-0 dhidi ya Coventry yaliyofungwa na Clint Dempsey (dk. 14 na dk. 37) na Gareth Bale (dk. 33). MATOKEO YA MECHI NYINGINE ZA KOMBE LA FA LEO Southampton 1 - 5 Chelsea Man City 3 - 0 Watford Tottenham 3 - 0 Coventry Wigan 1 - 1 Bournemouth QPR 1 - 1 West Brom Southend 2 - 2 Brentford Aldershot 3 - 1 Rotherham Aston Villa 2 - 1 Ipswich Barnsley 1 - 0 Burnley Blackburn 2 - 0 Bristol City Bolton 2 - 2 Sunderland Charlton 0 - 1 Huddersfield Crawley 1 - 3 Reading Crystal Palace 0 - 0 Stoke Derby 5 - 0 Tranmere Fulham 1 - 1 Blackpool Hull 1 - 1 Leyton Orient Leeds United 1 - 1 Birmingham Leicester 2 - 0 Burton Albion Luton 1 - 0 Wolves Macclesfield 2 - 1 Cardiff Middlesbrough 4 - 1 Hastings Utd Millwall 1 - 0 Preston Nottm Forest 2 - 3 Oldham Oxford Utd 0 - 3 Sheff Utd Peterborough 0 - 3 Norwich Sheff Wed 0 - 0 MK Dons |
No comments:
Post a Comment