MKURUGENZI
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Tanzania,Robert Manumba
amezidiwa kiasi cha kupumua kwa msaada wa mashine katika Hospitali ya
Aga Khan.
Habari
zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini
hapo baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo.
Taarifa
za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema kuwa tangu juzi, Manumba
alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo
ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
Manumba
amelazwa katika wodi ya wagonjwa mahututuzi (ICU) kwa ajili ya uangalizi
wa jopo la madaktari,taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi
zilizoifikia BLOG HII zinadai
kwamba Mkurugenzi huyo wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania amezidiwa
kiasi cha kupumua kwa kutumia mashine ya hewa safi ya Oxgen.
Habari
zilizopatikana jana zilieleza kuwa Manumba amelazwa hospitalini hapo
baada ya kusumbuliwa na maradhi kadhaa, ikiwamo figo,taarifa
za ndani kutoka Jeshi la Polisi zilisema jana kuwa tangu juzi, Manumba
alikuwa hajitambui baada ya kuugua malaria ghafla na hali hiyo
ilisababisha pia figo zake zote mbili kushindwa kufanya kazi.
“Alitakiwa
kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini ilishindikana kwa sababu
hajitambui, wakajaribu kumzindua, ikashindikana,” kilieleza chanzo hicho
cha habari ndani ya jeshi hilo. Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, alithibitisha kamishna huyo kulazwa ICU Aga Khan.
“Ni kweli amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, lakini hali yake inaendelea vizuri,” alisema Senso.
Mtu wa karibu na Manumba, alisema, Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya malaria, tatizo ambalo lilisababisha pia viungo vyake vingi, ikiwamo figo kushindwa kufanya kazi.
Daktari
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Dk Jaffer Dharsee alisema jana
kwamba Manumba alifikishwa katika hospitali hiyo tangu juzi akisumbuliwa
na malaria na alikuwa hajitambui.
“Nimepigiwa
simu nyingi leo (jana), nikiulizwa na watu mbalimbali wakitaka kufahamu
kama Manumba amefariki dunia, ninachotaka kuwaambia ni kwamba ni mzima
lakini yuko mahututi ICU"alisema Dk Dharsee.
No comments:
Post a Comment