Meza yetu ya habari imepokea taarifa fupi toka Mtwara usiku wa kuamkia leo ikitujuza kuchomwa moto kwa gari moja linalosadikiwa kutumika kwa biashara ya abiria (TAX) huko Mtwara. Chanzo chetu kimezidi kunyetisha kuwa mkasa huo unapewa mahusiano na sakata la GESI linaloendelea hivi sasa hapa nchini, kwani gari hiyo inasemekana lilitaka kumtorosha Bibi mmoja mkazi wa kijiji cha Msimbati - Mtwara aliyetoa ahadi kuwa gesi ikisafirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam kama serikali ilivyokusudia basi itageuka kuwa Maji na si gesi tena! Inasemekana bibi huyo alitaka kwenda kuonana na wazee wa kimila na kuongea na kuhusu suala zima la gesi, bado haijafahamika nini bibi huyo alitaka kujadili na wazee hao wa kimila.Hadi sasa haijajulikana nani kahusika na tukio hilo na haijajulikana kama kuna watu wameumia kutokana na tukio hilo.
WAZIRI MKUU RASMI MKUTANO WA KUMI WA WADAU WA LISHE.
-
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 03, 2024 anafunga mkutano wa Kumi wa
Wadau wa Lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Malaika Beach
Resort, J...
1 hour ago
No comments:
Post a Comment