skip to main |
skip to sidebar
KIKOSI CHA AZAM FC CHAWASILI SALAMA KENYA
Timu
ya Azam FC imewasili salama jijini Nairobi nchini Kenya jana usiku
tayari kwa kuanza michezo yake wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi
kwa ajili ya ligi kuu ya Tanzania mzunguko wa pili pamoja na mashindano
ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumzia program nzima ya
maandalizi kocha wa Azam FC, Stewart Hall amesema timu itacheza mechi
tatu za kirafiki na kufanya mzoezi ya siku mbili katika viwanja vya
Nyayo na City.
Alisema wachezaji wote wamefika salama, timu
itaacheza mchezo wake wa kwanza kesho ‘Jumamosi’ saa 3:30 (15:30hrs)
dhidi ya A.F.C Leopard, kwenye Uwanja wa Nyayo.
Azam FC leo ‘Ijumaa’ jioni itafanya mazoezi yake ya kwanza katika Uwanja wa Nyayo uliopo katikati ya jijini la Nairobi.
“Tutacheza michezo mitatu, michezo yetu itahusisha timu zenye viwango
vizuri katika ligi ya Kenya ambazo ni A.F.C Leopard, Sofapaka na K.C.B,
mechi hizo zitasaidia kuimarisha timu yangu” alisema Stewart.
Kocha Stewart alisema watafanya mazoezi na kucheza mechi katika viwanja
aina mbili vyenye nyasi za kawaida na zenye nyasi bandia kwa kuwa katika
michezo ya ligi viwanja hivyo vinaendana na mazingira ya Tanzania.
Azam FC iliyoko nchini hapa bila ya washambuliaji wake John Bocco na
Tchetche Kipre na mchezaji Waziri Salum wanaosumbuliwa na majeruhi, siku
ya Jumapili itacheza mechi yake ya pili ya kirafiki dhidi ya SOFAPAKA
kwenye uwanja huo huo.
Baada ya mchezo huo kikosi hicho
kitapumzika siku ya Jumatatu Jan 21, 2013 ambapo watatumia siku hiyo
kufanya mazoezi katika Uwanja wa City wenye nyasi bandia.
Azam FC
itamaliza safari yake ya maandalizi na mechi za kirafiki siku ya Jumanne
Jan 22 ambapo watacheza dhidi ya K.C.B kwenye Uwanja wa City mchezo
ambao utakamilisha safari hiyo ya siku saba.
Wachezaji walioko
jijini ni Mwadini Ally, Aishi Manula, Jackson Wandwi, Himid Mao, Samih
Haji Nuhu, David Mwantika, Luckson Kakolaki, Jockins Atudo, Michael
Bolou, Humphrey Mieno, Khamis Mcha, Gaudence Mwaikimba, Uhuru Selemani,
Brain Umony, Malika Ndeule, Omary Mtaki, Abdi Kassim ‘Babi’, Abdalah
Seif, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo na Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
No comments:
Post a Comment