Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 5, 2013

MAMBO YANAENDA HOVYO UWANJANI NA NYUMBANI KWA AGUERO - AACHANA NA MKEWE MTOTO WA MARADONA



Sergio Aguero ameachana na mkewe na Giannina, ambaye ni mtoto wa Diego Maradona, baada ya kudumu kwenye ndoa kwa miaka minne.

Giannina sasa anaaminika kwamba anaishi jijini Madrid na mtoto wao mwenye miaka mitatu Benjamin baada ya kuthibitisha kuachana kwake na Aguero kwenye mtandao wa Twitter.

Alisema 'tumeachana' kabla ya baadae kuongeza 'mwaka mgumu' na 'kumekuwepo na mabadiliko mengi'.

Kwenye Twitter, shabiki mmoja alimwambia Giannina: ‘Aguero hastahili kuwa nawe na mjinga' lakini akamjibu shabiki huyo 'Usiseme hivyo, ni baba wa mtoto wangu na hayupo kama ambavyo umesema.'

Sergio Aguero msimu amekuwa hayupo katika kiwango kizuri akiwa amefunga mabao nane tu na ligi ikiwa ipo katika awamu ya pili.

No comments:

Post a Comment