Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 6, 2013

NEWS ALERT:MH JOSEPH MBILINYI MBUNGE WA MBEYA MJINI HII NDO TAARIFA ALIYOIANDIKA KUPITIA MTANDAO WA FACEBOOK ISOME HAPA.

 TAARIFA: KUPITIA KATIBU WAO BWANA ENE,AWALI KABISA UMOJA WA BAJAJ MBEYA ULINIPA TAARIFA YA KUNITAKA NIWE MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI RASMI WA OFISI YAO ILIYOPO KATA YA ILEMI-MBEYA MJINI...LAKINI BAADAYE WAKANIPOTEZEA NA KUMUALIKA WAZIRI KILAZA MULUGO ALIYEENDA KUIFUNGUA OFISI HIYO JANA AMBAPO INASEMEKANA NI BAADA YA YEYE MULUGO KUWARUBUNI KWA KUWAPA FEDHA(LAKI SITA ) NA KUWAAHIDI FEDHA ZAIDI KUTOKA KWA BOSI WAKE KIKWETE BAADHI YA VIONGOZI WA BAJAJ ILI WAMUALIKE YEYE BADALA YA MIMI,JUST TO GET AT ME POLITICALLY!HII NI UKIACHA FEDHA ALIZOTOA HADHARANI KWA OFISI HIYO,LAKINI HILI HAPA MBEYA HALITUSUMBUI KWANI VIJANA HALISI WA BAJAJ WANAJUA NI NANI ANAYEWAPIGANIA WABAKI BARABARANI KUTAFUTA RIZIKI KILA SIKU BILA YA KUBUGHUDHIWA,KWA MFANO NI MIMI MBUNGE WAO NILIWAPELEKA NA KUWAPIGANIA KWA RPC NIKIAMBATANA NA VIONGOZI WAO SITA AKIWEMO KATIBU WAO ENE NA PIA M/KITI WAO WAKATI WALIPOKUWA WANAKAMATWA OVYO NA KUPIGWA FAINI KUBWA KILA WALIPOINGIA BARABARA KUBWA ZA HAPA MJINI,KERO AMBAYO HAIPO TENA KWAO HIVI SASA...

N.B: NAMSHAURI MULUGO NA MAGAMBA WENZAKE KUWA KWA HAPA MBEYA MJINI WATAMALIZA TU FEDHA ZAO LAKINI HAWATAPATA KITU,KWANI MBEYA MJINI HAINUNULIKI KWA FEDHA UMMA ULISHAAMKA HAPA...NA PENGINE NI VEMA ANGEPELEKA HIYO HELA JIMBONI KWAKE SONGWE AMBAKO WALIMU WANA KILIO CHA UKOSEFU WA CHAKI INGESAIDIA WATU WAKE NA PENGINE INGEMSAIDIA NA YEYE KISIASA....

No comments:

Post a Comment