MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana.
Kwa
mujibu wa King Sapeto, rafiki wa karibu wa marehemu, mazishi
yatafanyika Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam na kuanzia leo ndugu
na jamaa wa marehemu wanategemea ujumbe mzito kutoka kwa viongozi wa
Serikali watakaopishana kwenda kutoa mkono wa faraja kwenye nyumba ya
msiba.
Kwa
siku za hivi karibuni viongozi wa serikali na vyama mbali mbali vya
siasa wamekuwa mstari wa mbele kwa kushiriki bega kwa bega kwenye misiba
ya wasanii, hivyo watu wa karibu na Omari Omari wanategemea hali hiyo
pia itatokea kwa ndugu yao kipenzi. "Hatutegemi ubaguzi wa misiba"
anaeleza mmoja wa ndugu wa marehemu.
Omari
Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na
mstari mkali unaosema ndefu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa,
alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa
kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.
No comments:
Post a Comment