HUYU ndo MSANII WA BONGO FLAVOUR ALIYE FARIKI DUNIA ANAITWA OMARY OMARY ALIYEIMBA KUPATA MAJAALIWA.
MSANII nyota wa miondoko ya Mnanda a.k.a Mchiriku, Omari Omar amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Habari zilizoifikia , asubuhii zinasema kuwa, Omar Omar aliyetamba na nyimbo mbalimbali ukiwemo ule maarufu wa 'Kupata ni Majaliwa' alifariki nyumbani kwao Temeke, saa chache baada ya kurejeshwa toka hospitali ya temeke alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa.
Taarifa hizo zinasema kuwa mara baada ya kurejea nyumbani, msanii huyo alizidiwa na hatimaye kufariki na kwamba msiba wake upo nyumbani kwao Temeke Mikoroshini kwa ajili ya mipango ya mazishi.
Msiba wa msanii huo umekuja siku chache baada ya tasnia ya sanaa na burudani kumpoteza Juma Kilowoko 'Sajuki' msanii nyota wa filamu aliyefariki pia kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya muda mrefu.
dj sek blog inawamuombea kila la heri Omar Omar na wengine waliotangulia mbele ya haki mapumziko mema katika safari yao ya Ahera. Innallillah Waina Illah Rajiun.
Taarifa zaidi tutakuwa tunawaletea kujua mkali huyo wa mduara aliyewafanya wasanii wengine kufuata mkondo wake akiwemo Dogo Mfaume, Ferouz, Easy Man na wengine
SIKILIZA WIMBO WAKE -ANAITWA OMARY OMARY - MAJALIWA
Burudani : BSS Msimu wa 15 Wazinduliwa Rasmi
-
SHINDANO la kusaka Vipaji Tanzania Bongo Star Search 'BSS' misimu wa kumi
na tano umezinduliwa rasmi kwa sasa ni Bongo Star Search African wanavuka
boda...
RAIS MAGUFULI NA HISTORIA ISIYOFUTIKA
-
Na Emmanuel J. Shilatu
Kama ambavyo Watanzania tunavyomkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere kwa kusaidia ukombozi wa upatikanaji wa uhur...
-
*MAENDELEO BANK - PLC, inatarajia kufanya Mkutano mkuu wa 4 wa mwaka
Mkutano huo utakaowakutanisha Wanahisa wote utafanyika Juni 23 mwaka huu
kwenye ukum...
No comments:
Post a Comment