Wanafunzi
wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa
mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa
nne na nusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la
polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na
majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya
kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku
waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili
wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa.
Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
|
Ulinzi uliimarishwa nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.
|
Kamanda
wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman
Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara
baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo
aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo
walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
|
"Wanafunzi
wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa
kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo
unafanyika ubakaji huo"
|
Baadhi
ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye
kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda
Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.
|
Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.
|
Kova
akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa
baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote
kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.
|
Mitaani Posta.
|
Hadi kieleweke!
|
Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
|
Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.
|
Kwenye Kona ya feli kuwania geti ili waingie bure!
|
Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue!
|
Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria
|
Pamoja
na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na
kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani,
|
No comments:
Post a Comment