Jeshi
la polisi Kanda Maalum Dar es Salaam inawashikilia askari polisi watano
kwa tuhuma za upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 150 mara
baada ya tukio la uporaji lililofanyika eneo la Kariakoo mnamo tarehe
14/12/2012.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi,
Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova (pichani) amesema
baada ya tukio hilo zilipatikana taarifa kuwa fedha hizo zilipotea baada
ya mtuhumiwa Augustino Kayula na Frank John Mwangiba kukamatwa akiwa na
bastola aina ya Browing lakini hakuwa na fedha zilizoporwa, na ambaye
anasemekana ndiye aliyepora fedha hizo akiwa na wenzake.
Kamanda
Kova amesema pamoja na kukamatwa kwa askari hao pia wamekamatwa
majambazi wawili waliohusika na tukio hilo ambao ni ambao ni Deogratias
Kimaro mkazi wa Kilakala na Kulwa Mwakabala Mkazi wa Kijiwesamli wilaya
ya Ilala.
Watuhumiwa hao wote wanashikiliwa na upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na gwaride la utambulisho.
No comments:
Post a Comment