Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 19, 2013

SHIRIKA LA NSSF LAKABIDHIWA RASMI JENGO LAKE JIPYA JIJINI ARUSHA LILILOGHARIMU BILIONI 29 TOKA KWA MKANDARASI



DSCN7402Wataalamu wa ujenzi pamoja na wawakilishi wa Shirika la NSSF katika picha ya pamoja mara baada ya makabidhiano ya Jengo kubwa na la kisasa la shirika hilo lililojengwa Jijini Arusha, barabara ya Old Moshi. Jengo hilo lenye jumla ya ghorofa 15, mbili zikiwa chini (basement) kwa ajili ya maegesho ya magari linaelezwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 28.75 na limejengwa kwa muda wa miaka miwili.

Kamapuni ya China Jiangchang Engineering Co. Ltd (CRJE) ndiyo imekabidhi mradi huo ramsi hii leo baada ya kukamilika ujenzi wake uliowashirikisha pia wakandarasi wadogo 6 wa ndani.
Jiji la Arusha limepata muonekano mpya kwa kuongezewa jengo refu, kubwa na la kisasa kwa shughuli za kiosifi na biashara. NSSF nao wanategemea kuhamishia offisi zao kwa kanda hii katika jengo hili, halikadhalika huduma za kibenki zitapatikana hapo.
DSCN7392Sehemu ya mbele ya jengo, upande wa kushoto
DSCN7393Jengo jipya la Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (NSSF) lililoko Jijini Arusha, Barabara ya Old Moshi. Jengo hilo limekabidhiwa leo kwa shirika hilo toka kwa mkandarasi kutoka China ambae alishirikiana na wakandarasi wengine wa ndani.

No comments:

Post a Comment