STAA wa
filamu za Bongo, Shamsa Ford ametangaza simu yake ni ‘kimeo’, cha ajabu
msanii mwenzake, Jacqueline Wolper akatoa yake aina ya Blackberry na
kumkabidhi bila malipo Ishu hiyo ilijiri kwenye arobaini ya mama wa
Mtangazaji wa Kipindi cha Take One cha Clouds Tv, Zamaradi Mketema
ambapo Shamsa alionesha simu yake ilivyokuwa imechakaa na kufungwa kwa
‘rababendi’. Shamsa aliendelea kuomba msaada huo kwa kila msanii wa kike
aliyekuwa anaingia kwenye hitima hiyo ambapo alikuwa akipiga kampeni
kwa kusema kuwa ameshindwa kununua simu nyingine kutokana na kukosa
fedha kwa sababu ya majukumu kibao aliyonayo kwa sasa.
Muda
mfupi akiwa anaendelea na kuinadi ‘shida’ yake hiyo, aliingia Wolper
ambapo alikwenda kukaa karibu na Shamsa. Shamsa aliitumia fursa hiyo
kumueleza shida yake Wolper naye akatoa simu yake aina ya Blackberry na
kumkabidhi mbele ya wasanii wengine. Baada ya kupokea simu hiyo, Shamsa
alimshukuru Wolper kutokana na moyo wake wa upendo aliouonesha kwake.
Wasanii wengine waliokuwepo walibaki kumshangaa Wolper na kumwambia
Shamsa azidi kumshukuru mwanadada huyo kwani kilio chake kimeisha.
“Yaani namshukuru sana Wolper kwani amenileta tena kwenye ulimwengu wa
Blackberry kwa sababu nilikuwa nimepotea siku nyingi na sikuwa napata
habari mpya za mjini,” alisema Shamsa
DKT. NCHEMBA AKUTANA NA RAIS WA BENKI YA DUNIA AJAY BANGA
-
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (Kushoto),
akisalimiana na Rais wa Benki ya Dunia, Bw. Ajay Banga, kando ya Mkutano wa
Nishati ...
2 hours ago
No comments:
Post a Comment