Muuguzi wa zamu hospitali ya wilaya ya Masasi, Mkomaindo Fatuma Timbu amethibitisha kupokea maiti za watu saba.
Majeruhi
ambao idadi yao haijajulikana wamekimbizwa hospitali ya misheni ya
Ndanda kwa matibabu na hali bado ni tete Vurugu kubwa zilianza majira ya
saa 4 asubuhi leo baada ya polisi waliokuwa wakiendesha pikipiki
kumgonga mtu na kukataa kutoa ushirikiano,Hata hivyo hoja hiyo ilihamia
kwenye gesi na kundi la vijana mara moja walivamia nyumba ya mbunge wa
Masasi, Mariam kasembe na kuiwasha moto, pamoja na magari mawili.
Aidha
vijana hao walivamia nyumba ya Anna Abdallah na kuiteketeza kwa
moto,kabla ya kuivania ofisi ya CCM wilaya na kuichoma moto pamoja na
magari matatu.Hasira za wananchi hao zilifika kituo kidogo cha polisi
kilichopo Mkuti na kukichoma moto, baadae walichoma moto magari matano
ya halmashauri ya wilaya.
Pia walichoma moto ofisi ya elimu ya halmshauri ya wilaya Masasi vijijini, kabla ya kuichoma ofisi ya maliasili.
Polisi
kutoka maeneo mbalimbali yandani na nje ya mkoa inadaiwa walitumia
risasi za moto na kusababisha vifo vya watu Sita huku polisi akidaiwa
kuuawa kwa kupigwa na wananchi….
No comments:
Post a Comment