Mshambuliaji
wa Yanga, Jerry Tegete, 'Mkali wa Uturuki', akishangilia bao lake la
pili, huku kipa wa Tanzania Prisons, akishangaa akiwa chini baada ya
kushindwa kuokoa mpira huo uliopigwa na mkali huyo wa Uturuki. katika
dakika ya 82. ambapo bao la kwanza pia lilifungwa na mkali huyo na la
pili lilifungwa na Mbuyu Twite. Hadi mwisho wa mchezo huo Yanga
3-Tanzania Prisons 1.
Simon
Msuva, akipiga krosi, wakati wa mchezo huo wa fungua dimba ya Ligi Kuu
ya Tanzania Bara, mzunguko wa pili kwa upande wa timu hizo, uliochezwa
leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Didier Kavimbangu, akijaribu kutupia, wakati wa mchezo huo, ambapo shuti hilo lilipaa juu ya goli.
Sehemu
ya mashabiki wa Yanga, wakishangilia bao la tatu lililoizamisha Tanzania
Prisons na kuvunja matumaini ya kusawazisha na kuwafanya wachezaji wa
Prisons, kuanguka kila mara ambapo kila aliyekuwa akianguka alikuwa
ameshikwa na msuli.
Oscar Joshua, akijaribu kumfinya mchezaji wa Prisons.
Askari
Polisi wakimbeba Mlemavu kumtoa nje baada ya mlemavu huyo kuonekana
akikimbia huku akiwa hana nguo alipokuwa akijaribu kuingia katikati ya
uwanja, alipoulizwa mlemavu huyo alisema kuwa alikuwa akielekea
kumpngeza Mbuyu Twite, baada ya kuachia shuti kali lililomkuna vilivyo
na kutinga wavuni.
Seleka la kumbeba lilianza hivi.......
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, baada ya jioni hii kuitandika Prisons ya Mbeya mabao 3-1 katika
mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imetimzia pointi 32 baada ya kucheza
mechi 14, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi tano,
ikifuatiwa na Azam yenye pointi 27 na Simba 26.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa tayari zimefungana bao
1-1, Yanga wakitangulia kupata bao lao dakika ya 10 kabla ya Prisons
kusawazisha dakika ya 17.
Bao la Yanga lilifungwa na Jerry Tegete aliyeunganisha krosi
nzuri ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia, wakati la Prisons lilifungwa na Elias
Maguri, aliyeunganisha krosi nzuri ya Misango Magai kutoka wingi ya kushoto.
Tegete akiigusa nembo ya Yanga baada ya kufunga la tatu. PICHA ZAIDI BAADAYE. |
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na kasi nzuri kusaka ushindi
na iliwachukua dakika 11 tu kupata bao la pili, lililofungwa na Mbutu Twite
baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Prisons.
Wakati Prisons wakiwa kwenye jithada za kusaka bao la
kusawazisha, walijikuta wakitandikwa bao la tatu, Tegete tena akiwainua vitini
mashabiki wa Yanga, baada ya kupokea pasi nzuri ya Nurdin Bakari dakika ya 65.
Baada ya bao hilo, Yanga walianza kuonyesha vitu vya Uturuki
walipoweka kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko huu wa pili wa Ligi
Kuu, wakicheza soka ya madoido pasi nyingi, uzungu na kila aina ya mbwembwe,
ili mradi tu kuwaburudisha mashabiki wake.
Mapema kabla ya mchezo huo, kiungo wa Yanga, Frank Domayo alipatwa
na Malaria ya ghafla na kuenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akaanza
Nurdin Bakari, wakati mshambuliaji mpya wa Prisons, Emmanuel Gabriel
alienguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akachukua Elias Maguri, kwa
sababu ya kutokuwa na leseni ya TFF ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu. Suala la
leseni ya Gabriel, dhahiri ni uzembe wa viongozi wa Prisons.
Katika mchezo wa leo,
kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally
Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk 82, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Nurdin Bakari/David
Luhende dk 66, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza dk 64, Jerry Tegete na Haruna
Niyonzima.
TZ Prisons; David Abdallah, Aziz Sibo, Henry Mwalugala, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Nurdin Issa, Sino Augustino, Freddy Chudu, Elias Maguri, Misango Magai/John Matei dk58 na Jeremiah Juma.
No comments:
Post a Comment