Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 26, 2013

WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA CCM WASALIMIANA NA WANACCM MKOA WA TABORA, WANAENDELEA NA SAFARI KUELEKEA KIGOMA USIKU HUU


19Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdurahman Kinana akisalimiana na wanaCC, wa mkoa wa Tabora mara baada ya kuwasili katika kituo kikuu cha treni ya Reli ya Kati cha Tabora mjini. Abdurahman Kinana anaongoza wajumbe wa Sekretarieti ya CCM kuelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha Mapinduzi CCM yatakayofanyika kwenye uwaTanganyika Februari 3 mwaka huu.
5 Wananchi  wa Kituo cha Treni Salanda wakifanya biashara ya nyama ya kuku iria mbalimbali wanaosafiri na treni ya Reli ya Kati.
6 Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana akiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai mara baada ya kutika kituo cha Salanda Manyoni mkoani Singida ambapo wana CCM waliandaa mapokezi, kulia ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni John Chiligati
9 Wananchi wa Salanda Manyoni mkoani Singida wakiwa katika mapokezi hayo
10 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM , Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Rose Migiro katikati akicheza ngoma na wana CCM wa Singida.
11 Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na wana CCM wa Saland Manyoni Mkoani Singida wakati wajumbe wa Sekretarieti ya CCM walipopata mapokezi wakielekea mkoani Kigoma.
12Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana ili kuongea na Wana CCM wa mkoa wa Singida kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi.
13Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akiwasalimia wana CCM wa Mkoa wa Singida katika kijiji cha Salanda Manyoni Mkoani Singida leo.
14Katibu Mkuu CCM Abdurahman Kinana akipata mshikaki katika kijiji cha Salanda Manyoni wakati akielekea mkoani Kigoma kulia mbunge wa jimbo la Manyoni John Chiligati
15 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kulia na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha Rose Migiro wakipata nyama ya kuku kijiji cha Salanda mkoani Manyoni Singida.

No comments:

Post a Comment