KITUO cha Mabasi
yaendayo mikoani na nchi jirani (UBT), kinakabiliwa na vitendo vya
uhalifu, kutokana na sehemu kubwa kukosa umeme iliyosababishwa na
bomoabomoa ya kukihamishia Mbezi Luis.Wakizungumza na
Fullshangwe abiria na waangalizi wa mbasi kituoni hapo, walisema
unapofika usiku hali inakuwa ya kutisha kutokana na giza totoro ambalo
linawashawishi vibaka kuvamia eneo hilo.
Walisema miongoni mwa uhalifu
unaofanywa na vibaka hao, ni kuibiwa mafuta kwenye mbasi, vyuma vya
majengo yaliovunjwa na kuporwa abiria wanaofika usiku.
Alisema kabla kituo hakijavunjwa
kila mfanyabiashara alikuwa na mlinzi wake, hivi sasa eneo hilo liko
wazi kitendo kinachosababisha wezi kuongezeka.
“Usiku mnatisha unajua magari
yenyewe yanatisha yanapokuwa mengi, hakuna mwanga kitendo kinchochochea
wezi kupata maeneo ya kujifisha na kufanya vitendo vya uhalifu”alisema
mmoja wa waangalizi wa magari hayo.
Naye James John, alisema kwa
sasa kituo chote hakina umeme ukiondoa, jingo la polisi hali ambayo
inasababisha huduma zote usiku kuwa duni hata ile sehemu ya kupunzikia
wasafiri na vyoo ambavyo ni muhimu kwa wasafiri, ambako nako kuna giza.
“Tabu inakuwa alfajiri pale
wasafiri wanapofika kituoni hapo, kwani inatuwia vigumu kubaini haraka
magari tunayosafiri nayo kutokana na giza”alisema John.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa Jiji Mussa Zungiza ili kutoa ufafanuzi, ilielezwa kuwa yuko safarini nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment