Magolikipa Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul wakiwa katika mazoezi ya asubuhi leo nchini Uturuki |
Wachezaji
na bechi la ufundi la timu ya Young Africans wamefurahishwa na hali ya
kambi hapa katika mji wa Antalya kwamba hali ya hewa ni nzuri, vyakula
aina zote vinapatiikana na huduma za mazoezi kwa ajili ya kambi ni za
kiwango cha juu sana.
Wakiongea
na www.youngafricans.co.tz Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli
hali ya hewa sio mbaya kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya
hewa ni nzuri, mazingira ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili
ya mazoezi vipo kwa wingi hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu
kuwaelekeza wachezaji wafanye nini.
Kocha
Siwa amesema pia wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua
kuileta timu kambini nchini Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi
nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo ambayo hayana bughuza kwani kambi
ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu nyingi za Ulaya
zinapenda kuja kuweka kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.
Fred
Felix Minizro kocha msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa
ujumla ni nzuri, na kuhusu hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya
na Arusha hivyo haoni kama hali ya hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika
kambi hii ya mafunzo.
Naye
kiungo mshambuliaji Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii
ya kuja kuweka kambi nchini Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z
akambi ni nzuri kabisa hivyo wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu
Brandts na pindi watakaporudi Tanzania wataweza kuwapa raha wapenzi wa
soka kwa kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa kipindi cha wiki mbili.
No comments:
Post a Comment